KINDA wa Manchester United, Adnan Januzaj amepokea vitisho vya kuuawa kwa sababu ya kuamua kuichezea Ubelgiji, taarifa zimesema nchini Serbia.
Mchezaji huyo wa umri wa miaka 19 alikuwa anaweza kuchezea Serbia, Uturuki, Albania, Kosovo na hata England baadaye, lakini akaamua kuchezea nchi aliyozaliwa Aprili mwaka huu, akiichezea mechi ya kwanza rasmi dhidi ya Tunisia kiasi cha wiki moja kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia nchini Brazil.
Taarifa za kituo cha Redio ya Serbia, S Media na gazeti la Ubelgiji la Het Nieuwsblad, zimesema kwamba Januzaj ametishiwa lifo na aria wa Kosovan-Albania wenye hasira kwa uamuzi wake wa kuwakana
Indaiwa walimkanya kutoikana Kosovo, ambako familia yake iliishi kabla ya kuhamia Ubelgiji mwaka 1992.
Januzaj alicheza kwa saa moja tu Kombe la Dunia nchini Brazil, akianza katika mchezo wa mwisho wa Ubelgiji dhidi ya Korea Kusini, kabla ya timu hiyo kutolewa na Argentina katika Robo Fainali.
Post a Comment