Mafundi wakiwa kazini katika chumba cha
Independent Power Tanzania Limited (IPTL) cha uendeshaji mitambo.
Malori yakisubiri kushusha mafuta mazito
yanayotumika na kampuni ya kufua umeme ya IPTL, ambayo umeme wake huingizwa
katika gridi ya taifa
Sehemu ya mitambo ya kufua umeme ya kampuni ya
IPTL
Sehemu ya kituo cha kusambaza umeme kutoka katika
mitambo ya kampuni ya kufua umeme ya IPTL
MAKAMPUNI
ya Songas Tanzania na Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ni makampuni
pekee ya binafsi yazalishayo umeme ambayo kwa sasa uzalisha umeme kwa ajili ya
gridi ya Taifa wakati mengine yaliyobaki Aggreko na Symbion Power Tanzania
yakiwa yanatumika tu wakati wa dharura.
Uwezo
ulioongezwa katika mitambo ya gesi asilia ya Songas iliyopo Ubungo ni ya
megawati 189, wakati kampuni ya IPTL inatumia mafuta mazito na uwezo wake ni
kuzalisha megawati 103, ingawa uzalishaji huo ubadilika mara kwa mara kutokana
na mahitaji katika gridi ya Taifa.
Kaimu
Meneja Uhusiano wa Tanesco, Bw. Adrian Severin alisema hii ni kutokana na
ukweli kuwa nchi kwa sasa inazalisha
umeme kutoka katika vyanzo vingine vyenye gharama nafuu ambavyo ni maji na
nishati ya mvuke (thermal power).
“Mitambo
ya uzalishaji umeme kupitia maji kwa sasa inazalisha kati ya megawati 450 hadi 500
toka katika mitambo yenye uwezo wa megawati 561.84 wakati mitambo mitatu ya
gesi inayomilikiwa na Tanesco katika eneo la Ubungo na Tegeta inazalisha jumla
ya megawati 252.
“Hii
inafanya jumla ya uzalishaji kutokana na maji na nishati ya mvuke kuwa megawati
752 ambayo inatosheleza mahitaji katika gridi ya taifa. Mahitaji makubwa ya
umeme Tanzania mara ya mwisho yalirekodiwa kuwa megawati 898.5,” alibainisha
Bw. Severin.
Uzalishaji
wa pamoja kwa Symbion ni megawati 120 ambapo uzalisha megawati 60 toka katika
mafuta aina ya Jet – 1 na nyingine megawati 60 kupitia gesi asilia, wakati
Aggreko inazalisha megawati 100 kwa kutumia mafuta mazito katika mitambo yake
iliyopo Ubungo na Tegeta jijini Dar es Salaam. Hata
hivyo, Bw. Severin alisema kuwa mitambo ya Symbion na Aggreko kwa sasa itatumika
tu katika hali ya dharura itakapotokea.
“Katika
hali ambayo kina cha maji katika mitambo yetu inayozalisha nishati kupitia maji
kimepungua au pale ambapo mitambo yetu inayozalisha nishati ya mvuke inafanyiwa
ukarabati, uwa mara nyingi tunawaomba Aggreko na Symbion kuingiza umemewao
katika gridi ya taifa ili pasiwepo na adha ya mgao,” Alisema Bw. Severin.
Akizungumza
kwa njia ya simu jana juu ya kwa nini anadhani kampuni yake inaendelea
kuzalisha umeme katika gridi ya Taifa, licha ya mitambo yake kutumia mafuta
mazito ambayo imeongeza gharama za uzalishaji, Mwenyekiti Mtendaji wa IPTL, Bw.
Harbinder Sethi alisema IPTL chini ya uongozi wa Pan Africa Power Solutions
(PAP) imejitoa katika hali ya kupata faida kubwa ya kupindukia, kwa kuanza kufanya
uendeshaji wa gharama nafuu ikiwa na lengo la kuipatia nchi (wateja) umeme wa
bei nafuu.
“Ni
kweli kuwa uzalishaji wa nishati kwa kutumia mafuta mazito ni ghali na ndiyo
sababu tuna mpango wa kuweka mitambo ya gesi ya megawati 200 pembezoni mwa IPTL
katika awamu ya kwanza ya mkakati wetu wa upanuzi. Majadiliano yanaendelea na
mamlaka zote zinazohusika. Lengo ni kuhakikisha kuwa watanzania wote wanapata
nishati ya bei rahisi katika ukanda wa Afrika mashariki na kati na kuwafikia
watu wengi zaidi hivi karibuni,” alisema.
Bw.
Sethi alionyesha kuwa na matarajio kwamba mabadiliko yaliyoletwa na PAP ndani
ya IPTL, itaisaidia kampuni hiyo kuchangia kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko
ya hali ya umeme iliyopo na unafuu wa gharama zake nchini.
Vyanzo
vya nishati kupitia nguvu ya maji nchini ni pamoja na Kidatu megawati 204,
Kihansi megawati 180, Mtera megawati 80, Nyumba ya Mungu megawati 8, New
Pangani megawati 68 na vile vile Hale megawati 21.
Kwa
upande mwingine, Tanesco inaendesha mitambo miwili ya gesi iliyopo Ubungo kwa
pamoja ikizalisha umeme wa megawati 207 pamoja na mtambo mmoja wa gesi uliopo
Tegata wenye uwezo wa kuzalisha megawati 45 na mtambo mwingine ukitumia mafuta
ghafi mazito uliopo Nyakato, Mwanza wenye uwezo wa kuzalisha megawati 63.
Post a Comment