Wizara ya
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, limetoa mwezi mmoja kwa watumishi wake
wote kuwasilisha vyeti vyao ili viweze kufanyiwa uhakiki ili kubaini
kama kuna vyeti feki.
Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo, Job Masima, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati wa
Mafunzo ya Elimu ya Hifadhi ya Jamii yaliyoandaliwa na Mamlaka ya
Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).
Alisema
kuanzia jana, watumishi wote waliopo chini ya Wizara hiyo watapaswa
kuwasilisha vyeti vya vyuo walivyosomea."Natoa mwezi mmoja kuanzia leo
hadi Januari, wawasilishe yeti vyao wizarani viweze kukaguliwa...baada
ya ukaguzi tutafuatilia maeneo waliyosomea ili kubaini kama kuna askari
wanaotumia vyeti feki," alisema.
Alisema
askari ambao watabainika kutumia vyeti feki na kupata vyeo wakiwa
kazini, watashushwa vyeo ambapo lengo a ukaguzi huo ni kuwataka
watumishi hao kusomea katika vyuo vinavyotambulika na Serikali si vya
mitaani.
Aliongeza
kuwa, mpango huo pia utawahusisha watumishi ambao wamesomeshwa na Wizara
ambao nao watatakiwa kwasilisha vyeti vyao upya.Kwa upande wake,
Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka, aliwataka watumishi wa Wizara
hiyo kujiunga na Mifuko ya Hifadhi za Jamii kwa ajili ya kuweka mafao
yao.
Alisema kuna
mifuko mingi hivyo kila mtumishi anaweza kuchagua wowote anaopenda
kujiunga nao ili uweze kumsaidia dhidi ya matukio yasiotarajiwa.Matukio
hayo ni pamoja na maradhi, ulemavu, kustaafu kazi,kuacha kwa hiari au
kwa lazima. Akizungumzia changamoto zilizopo katika sekta hiyo, alisema
takwimu zinaonyesha wananchi walio katika sekta rasmi wanakadiriwa
kufikia milioni 1.5 ndio wananufaika na sekta hiyo.
Post a Comment