Mchezaji wa Arsenal(kushoto) akipambana na mchezaji wa Basiktas(kulia). Arsenal ilishinda 1-0
Asernal
imefuzu kucheza fainali za kombe la UEFA kwa msimu wa 17 mfululizo
baada ya kuichabanga Besiktas ya Uturuki kwa jumla ya goli 1-0.
Katika mchezo wa awali wiki moja iliyopita, timu hizo zilitoka sare ya kutofungana.
Hata
hivyo, mchezaji mpya aliyejiunga na Arsenal msimu huu, Alexis Sanchez
ndiye aliyeiwezesha Asernal kusonga mbele baada ya kufunga goli la
kwanza tangu ajiunge na Arsenal akitokea Barcelona mwezi mmoja uliopita.
Sanchez
aliyenunuliwa kwa kitita cha pauni milioni 35 kutoka Barcelona kwa
kipindi chote cha mchezo alihaha kutafuta goli, ambapo katika dakika
moja ya nyongeza katika kipindi cha kwanza cha mchezo aliweza
kutumbukiza kimiani goli pekee kwa Arsenal na kufuzu kutoka hatua ya
makundi kucheza fainali za UEFA kwa mwaka huu.
Arsenal
ilipata nafasi za kumaliza mchezo mapema, lakini wachezaji wake Santi
Cazorla na Alex Oxlade-Chamberlain walipoteza nafasi nyingi za wazi
walizopata.
Zikiwa
zimebaki dakika 15 kumaliza mchezo kipindi cha pili, Arsenal ilipata
pigo baada ya mlinzi wake wa kulia Mathieu Debuchy alitolewa nje kwa
kadi nyekundu kutokana na kuonyeshwa kadi mbili za njano. Lakini Arsenal
waliendelea kupambana hadi dakika ya mwisho ya mchezo.
Timu
nyingine zilizofuzu kucheza fainali za UEFA kwa mwaka huu katika michezo
ya Jumatano usiku ni Athletic Bilbao iliyopata ushindi wa magoli 3-1
dhidi ya Napoli. (Jumla 4-2), Bayer 04 Leverkusen 4, FC Copenhagen 0,
jumla(7-2).
Ludogorets Razgrad 1 - 0 Steaua Bucharest
Malmö FF 3 - 0 FC Red Bull Salzburg


Post a Comment