Jaji
Kiongozi Shaban Ally Lila akihutubia katika uzinduzi wa Bodi mpya ya
Baraza la Habari Tanzania kwa niaba ya Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman
kwenye Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam, Agosti 7,2014.
Rais
wa Baraza la Habari aliyemaliza muda wake Jaji Mstaafu Dk. Robert
Kisanga akihutubia katika uzinduzi wa Bodi mpya ya Baraza la Habari
Tanzania ambapo alisisitiza umuhimu wa Baraza la habari na kutaka
liungwe mkono kufanikisha malengo yake .Dar es Salaam, Agosti 7,2014.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Habari Kajubi Mukajanga akizungumza wakati wa
kutambulisha Bodi mpya ya Baraza la Habari Tanzania kwenye Hoteli ya
Blue Pearl Dar es salaam,Agosti 7,2014.
Baadhi ya wageni waalikwa na waandishi wa habari wakiwa katika uzinduzi wa Bodi mpya ya Baraza la Habari Tanzania.
Meneja
wa Udhibiti na Viwango wa Baraza la Habari Tanzania Pili Mtambalike
(Kushoto) akifuatiwa na Meneja wa Rasilimali Watu wa Baraza la Habari
Tanzania Ziada Kirobo, Meneja wa Fedha wa Baraza la Habari John Nguya na
Mjumbe mpya wa Bodi ya Baraza la Habari Tanzania Profesa Bernadetha
Killian wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo.
Rais
wa Baraza la Habari Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akipokea cheti cha
kumaliza muda wa kutumikia Bodi iliyomaliza muda wake kutoka kwa Jaji
Kiongozi Shaban Ally Lila .
Rafii
Haji Makame mjumbe wa Bodi iliyomaliza muda wake akionyesha cheti
alichokabidhiwa katika sherehe za kuaga bodi ya zamani na kuzindua bodi
mpya ya Baraza la Habari, kulia ni Jaji Kiongozi Shaban Ally Lila na
kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Kajubi Mukajanga.
Jaji
Kiongozi Shaban Ally Lila akimkabidhi cheti Mjumbe wa Bodi iliyomaliza
muda wake Ussu Mallya wakati wa sherehe za kuzindua Bodi Mpya na kuiaga
ya zamani kwenye Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es salaam.
Jaji
Kiongozi Shaban Ally Lila akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa Bodi mpya
ya Baraza la Habari Tanzania Ndugu Badra Haji Masoud wakati wa uzinduzi
wa Bodi hiyo.
Baadhi
ya Wajumbe wa Bodi mpya ,wajumbe waliomaliza muda pamoja na wageni
waalikwa wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa Bodi hiyo .
Jaji Kiongozi Shaban Ally Lila akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi mpya ya Baraza la Habari Tanzania.
Wajumbe
wa Bodi Mpya na iliyomaliza muda pamoja na wageni waalikwa wakiwa
katika picha ya pamoja mgeni rasmi katika uzinduzi wa bodi mpya Jaji
Shaban Ally Lila (wa tatu kusoto walioketi) Picha kwa Hisani ya Adam H. Mzee wa kamerayangublog.com
Post a Comment