Bunge
Maalum la Katiba limepitisha azimio la mapendekezo marekebisho ya
baadhi ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba ili kuwezesha ili kuwezesha
kijadili Rasimu ya Katiba kwa muda siku 60 za nyongeza na tatu
zilizobakia.
Marekebisho
hayo yamepitishwa kufuatia Mwenyekiti wa Kanuni na Haki za Bunge
Maalum la Katiba, Mhe. Pandu Ameir Kificho kuwasilisha mapendekezo ya
kanuni hizo mapema leo asubuhi katika Bunge hilo mjini Dodoma mara
baada ya kuanza kikao cha 30.
Azimio
hilo,limepitishwa baada ya baadhi ya wajumbe kuchangia hoja hiyo na
kuungwa mkono, ambapo uamuzi huo ulitangaza na Mwenyekiti wa Bunge hilo,
Mhe. Samuel Sitta.
Mhe
. Sitta alisema Bunge hilo ,litaanza kujadili rasimu ya Katiba Mpya
katika kamati 12 kuanzia kesho tarehe 6 Agosti, mwaka huu kwa muda wa
siku 15 yaani hadi Agosti 27, mwaka huu.
“
Hivi sasa watumishi wa Bunge na Sekretarieti wanaweka nyezo zote za
kupitia , ambapo pia Katibu wa Bunge Maalum la Katiba yupo nao
anashughulikia suala hili pamoja na kamati ndogo ili kuwezesha kazi hii
kufanyika bila buguza,” alisema Mhe. Sitta.
Aliongeza kwamba baada ya hapo kutakuwa na siku tatu kwa kamati kukamilisha Rasimu zao za Katiba.
“
Kamati zinatakiwa kutumia sekretarieti ndogo kuandika sura wasisubiri
hadi Agosti 28,mwaka huu. Tumeongeza Idadi ya wataalamu katika kila
sekretarieti ndogo,” alisisitiza.
Aidha
Mhe. Sitta alisema kutokana na marekebisho ya Kanuni ya 32 kifungu cha
2 kinachosema kamati kubadilisha sura za rasimu na sura, hivyo
zinatakiwa kutumia muda wa siku saba kupendekeza sura mpya kuanzia
Agosti 6,mwaka huu hadi Agosti 13,mwaka huu.
Akizungumzia
kuhusu maudhurio ya wajumbe wa Bunge hilo, alisema watakiwa kutia saini
kwenye maudhurio hayo na hakuna kusainiana kila mtu atatia saini
mwenyewe.
Mhe .Sitta akifafanua kuhusu utaratibu wa kutoa taarifa za kamati kwa vyombo vya habari alisema utatolewa.
Alisema Bunge hilo litarejea Septemba 2, mwaka huu baada ya kukamilisha kazi za kamati.
Bunge hilo limeanza vikao vyake kwa mara nyingine leo, baada ya kuairishwa Aprili 25, mwaka huu.
Post a Comment