Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), umemchagua Rais wa Chama cha Walimu (CWT), Gratian Mukoba, kuwa Rais wa shirikisho hilo katika uchaguzi uliokwenda raundi mbili, baada ya raundi ya kwanza kukosa mshindi.
Katika
raundi ya kwanza, kura zao zilishindwa kutimia baada ya kila mgombea
kwenda chini ya nusu ya idadi ya wajumbe wa mkutano huo mkuu wa Tucta.
Katika marudio, Mkoba alimbwaga mgombea mwenzake, Baraka Igangula kwa kupata kura 172 wakati mpinzani wake alipata kura 110.
Akizungumza
baada ya kutangazwa mshindi, Mkoba alisema anashukuru kwa kupata
ushindi huo, kwani anatambua changamoto zilizopo za wafanyakazi.
Alisema yeye binafsi kwa kushirikiana na uongozi, watahakikisha wanawatumikia wafanyakazi kwa uwezo wao wote.
Mkoba
alisema atahakikisha anarudisha imani kwa wafanyakazi, kama alivyoahidi
katika kampeni zake na kikubwa ni ushirikiano ili waweze kufanikiwa.
Kwa upande wake, Igangula aliwataka wafanyakazi kuungana kwa pamoja
kujenga shirikisho.
Mkutano huo pia ulimrejesha katika kazi yake Katibu Mkuu wa TUCTA, Nicholaus Mgaya.
Awali,
wakati wa mkutano huo ukiendelea, wajumbe wa kutoka Chama cha
Wafanyakazi wa Viwandani, Biashara,Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri
(TUICO) walisusa uchaguzi wa kumpata rais wa shirikisho hilo.
Wajumbe
hao walisusa uchaguzi huo, wakiongozwa na Rais wao, Omary Ayuob Jumaa
kwa madai kuwa Shirikisho limekataa kurudisha jina la rais huyo ili awe
miongoni mwa wagombea wa nafasi hiyo.
Uchaguzi
huo ambao waandishi wa habari hawakuruhusiwa, ila mpaka baada ya
uchaguzi, ulisimamiwa na Profesa Hamza Tiko na kufunguliwa na Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi ambaye aliwaasa kufanya uchaguzi kwa
utulivu na amani.
Post a Comment