Nini kinaendelea? Video Queen wa Bongo anayeshikiliwa na jeshi la polisi nchini China kwa msala wa madai ya kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’, Jacqueline Fitizpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ anadaiwa kuyeyuka gerezani.
Kwa mujibu wa ‘mtu wetu’ aliyeambatana
na rafiki zake Jack kwenda kumuona gerezani, Macau, Hong Kong nchini
humo, walijikuta wakipigwa na butwaa kuambiwa hakuna mtu kama huyo
gerezani hapo hivyo kuibua hofu kuwa huenda amenyongwa.
Uchunguzi wetu gerezani hapo ulibaini
kwamba tofauti na hofu ya rafiki zake, kuna uwezekano Jack amehamishiwa
gereza lingine lililopo nje kidogo ya Mji wa Macau.Chanzo chetu hicho
kilidai kwamba habari za ndani zilieleza kwamba Jack amehamishwa gereza
hivyo kwa maelezo zaidi watu wanaokwenda kumtembelea waende kwenye ofisi
za gereza hilo alilokuwa awali watapewa maelekezo wapi alipo mtu wao.
“Unajua watu wanaokwenda kumtembelea
Jack gerezani ni Watanzania walioko huku China kwa shughuli maalum hasa
za sanaa, kama vile sarakasi au maigizo, wengine wote wanaogopa, wanajua
wanaweza kukamatwa.
“Tulipokwenda na mazagazaga yetu
tuliambiwa Jack amehamishwa gereza na inaonekana aliomba mwenyewe ila
hatujui ni kwa nini alifanya hivyo,” kilisema chanzo hicho.Hivi karibuni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, John Haule alitoa taarifa na
kutaja jumla ya watuhumiwa waliokamatwa kwa kesi za madawa ya kulevya
ambapo alisema kuwa kuna Watanzania wengi wapo kwenye magereza
mbalimbali China.
“Katika magereza ya China hadi Februari
(mwaka huu) tulipewa taarifa kwamba wapo Watanzania 177 magerezani na
kati ya hao 15 wamehukumiwa kunyongwa kutokana na baishara hiyo ya
madawa ya kulevya,” ilisema taarifa hiyo ya katibu mkuu.
Jack alikamatwa Macau, Hong Kong, mwaka
jana hivyo kesi yake inaendelea kuunguruma. Tofauti na Beijing ambao
huwa wananyonga watu wanaojishughulisha na unga, Hong Kong ni kifungo
cha miaka kadhaa tu.
Post a Comment