Jux akiwa na Jack Patrick.
Jux ambaye anasoma nchini China huku
akifanya muziki wa Bongo Fleva, alifunguka hayo juzikati katika
‘exclusive interview’ aliyoifanya na paparazi alipokuwa mjini Kahama
alipokwenda kwenye Serengeti Fiesta 2014.
Akijibu swali la paparazi lililomtaka
afungukie penzi lake na Jack ambalo alikuwa akichengachenga kila
alipotakiwa kutoa ufafanuzi na vyombo vya habari, Jux alianza kwa kukiri
kwamba mrembo huyo alikuwa mpenzi wake na walidumu kwa takriban miezi
saba kabla hajakutwa na msala wa madawa ya kulevya.
Alisema tangu aanze kuyajua mapenzi,
Jack alikuwa ni mwanamke wa pekee kwake ingawa wakati anapatwa matatizo
walikuwa wametibuana kwa kipindi cha wiki mbili.
“Nilisikitika sana niliposikia
amekamatwa kwa madawa ya kulevya, nilikuwa sijui kama anafanya hiyo
biashara na kinachoniumiza zaidi ni kwamba nilikuwa najua yupo Bongo na
nikajua tutaonana maana mimi nilikuwa Bongo wakati huo,” alisema Jux.
Alipoulizwa kama ana taarifa za Jack
kufungwa miaka sita jela kama ilivyoripotiwa wiki iliyopita, Jux alisema
hana taarifa hizo.“Kiukweli sijazipata habari hizo labda nitakapoenda
tena China ndiyo nitajua kupitia kwa mwanasheria wake maana kwa sasa
hajanipa taarifa na hana namba yangu ya simu ya hapa,” alisema Jux.
Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana
akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1
katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea jijini Bangkok nchini Thailand
kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China.




Post a Comment