Teknolojia inazidi kukua na watu hawajaridhika kabisa na kile kinachoonekana duniani kuwa ni mageuzi.
Mjasiriamali
wa Marekani ambaye ni mzaliwa wa Afrika Kusini, billionaire Elon Musk
ambaye amegundua teknolojia ya mwendo kazi wa hali ya juu ‘The Hyper
loop’ amekuja na wazo la kuunda treni ambayo itakuwa na mwendo mara
mbili ya mwendo kasi wa ndege za kawaida.
Mara
tu treni hiyo itakapotengenezwa kwa teknolojia hiyo ya mwendo kasi,
itakuwa na uwezo wakuondoka mara tu abiria watapokuwa ndani ya treni
hiyo kwa idadi inayotakiwa bila kusubiri ratiba baalum kama ilivyo kwa
treni za umeme nchini Marekani.
Elon
Musk ameeleza kuwa endapo teknolojia hiyo itakubalika na kupitishwa
chombo hicyho kitakuwa na uwezo wa kubeba abiria kutoka Los Angeles hadi
San Francisco ndani ya nusu saa tu!! Mwendo ambao kwa kawaida ndege
hutumia zaidi ya saa moja. inaweza kutoka New York hadi China kwa muda
wa saa mbili tu.
Kwa
maelezo ya Elon Musk, wengi wanamuona kama amechanganyikiwa na pesa
hivi lakini baadhi ya engineers wanaonekana kuiamini idea yake kwa kiasi
fulani hasa baada ya kuona vifaa alivyonavyo na kuelekeza jinsi
itakavyofanya kazi.
TAZAMA VIDEO HAPA
Sh
Post a Comment