Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, baada ya kushauriana na Tume ya
Utumishi wa Mahakama, amewateua wafuatao kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuanzia tarehe 13 Agosti, 2014.
WATUMISHI WA MAHAKAMA
(i) Bw. Penterine Muliisa KENTE, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani, Dar es Salaam.
(ii) Bw. Benedict Bartholomew MWINGWA, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam.
(iii) Bw. Edson James MKASIMONGWA, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Katibu wa Jaji Mkuu.
(iv) Bw. David Eliad MRANGO, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msajili, Baraza la Ushindani, Dar es Salaam.
(v) Bw. Mohamed Rashid GWAE, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msajili, Mahakama Kuu, Kitengo cha Kazi, Dar es Salaam.
(vi) Dkt. John Eudes RUHANGISA, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msajili, Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Arusha.
(vii) Bw. Firmin Nyanda MATOGORO, ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Naibu Mwenyekiti, Baraza la Rufaa la Kodi, Dar es Salaam.
MAWAKILI WA SERIKALI NA TAASISI MBALIMBALI ZA SERIKALI
(i) Dkt. Eliezer Mbuki FELESHI, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi wa Mashitaka, Dar es Salaam.
(ii) Bi. Barke Mbaraka Aboud SEHEL, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam.
(iii) Bi. Winfrida Beatrice KOROSSO ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Katibu Mtendaji, Tume ya Kurekebisha Sheria, Dar es Salaam.
(iv) Bi. Lilian Leonard MASHAKA, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (TAKUKURU), Dar es Salaam.
(v) Bi. Leila Edith MGONYA, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msaidizi wa Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dar es Salaam.
(vi) Bw. Awadhi MOHAMED, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Mchunguzi Mkuu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (TAKURURU), Dar es Salaam.
MAWAKILI WA KUJITEGEMEA
(i) Bw. Lugano J.S. MWANDAMBO, kutoka REX Attorneys, Dar es Salaam.
(ii) Bw. Amour Said KHAMIS, kutoka AKSA Attorneys, Dar es Salaam.
(iii) Dkt. Paul KIHWELU, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Wakili wa Kujitegemeana na Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu Huria, Dar es Salaam.
(iv) Bi. Rose Ally EBRAHIMU, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Wakili wa Kujitegemea, Bulyankulu Gold Mine Ltd, Shinyanga.
(v) Bi. Salma MAGHIMBI, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Mjumbe, Tume ya Ushindani, (FCC), Dar es Salaam.
WATUMISHI WA VYUO VIKUU
(i) Dkt. Mary Caroline LEVIRA, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha.
(ii) Dkt. Modesta Opiyo MAKOPOLO, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu, Mzumbe, Morogoro.
Wateuliwa wote wataapisha tarehe 15 Agosti, 2014 Saa 05.00 asubuhi katika Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam.
Imetolewa na Mkurugenzi Idara ya habari Maelezo
13 Agosti, 2014
Post a Comment