Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika mkutano
wa Watanzania wanaoishi ughaibuni (Diaspora) ambao umepangwa kufanyika katika Hoteli
ya Serena jijini Dar es Salaam tarehe 14 na 15 Agosti 2014.
Mkutano huo ambao umeandaliwa kwa
ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taasisi ya
Diaspora Tanzania (Tanzania Diaspora Initiative-TDI), unalenga kuwahamasisha Watanazania
wanaoishi ughaibuni wenye utaalamu na mitaji kurudi nchini au kuwekeza katika shughuli
mbalimbali kwa madhumuni ya kukuza uchumi wa nchi.
Aidha, Mkutano huo ambao ni wa kwanza
kufanyika nchini, wenye kaulimbiu “Unganisha, Shiriki, Toa taarifa na Wekeza” (Connect,
Engage, Inform and Invest) utatoa nafasi kwa washiriki kutambua vyema fursa za
uwekezaji na ajira zinazopatikana Tanzania.
Imetolewa
na: Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es salaam.
13 Agosti, 2014
Post a Comment