JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
TAARIFA
KWA UMMA
SEMINA YA UTHAMINISHAJI MADINI KUFANYIKA
BAGAMOYO
Wizara ya Nishati na
Madini kupitia Kitengo cha Uthamini wa Madini ya Almasi na Vito (TANSORT) inatarajia kufanya semina ya siku mbili ambayo itahusisha Makamishna Wasaidizi wa Madini
wa Kanda na Afisa Madini Wakazi yenye lengo la kujadili
utendaji kazi, mafanikio pamoja na maboresho ya tasnia ya vito na almasi nchini.
Semina hiyo itakayofunguliwa
na Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Eliakim Maswi, inatarajiwa kuanza Agosti
14, 2014 na kumalizika Agosti 15, 2014.
TANSORT
itaendesha semina hiyo ili kuboresha
shughuli za uthamini wa almasi na madini
ya vito kwa lengo la kukokotoa
mrabaha, kutayarisha miongozo ya bei za
madini zinazotumika kukokotoa mrabaha,
kutoa huduma za kijemolojia ( Gemological
Services) kwa wachimbaji wadogo na wa kati, kusimamia mauzo ya almasi na
madini ya vito ndani na nje ya nchi.
Semina hiyo
itawawezesha washiriki kutoa maoni yatakayowezesha Kitengo hicho kuboresha huduma za kutoa ushauri wa masoko, ukataji na
ukadiriaji thamani kwa wachimbaji
wadogo na wa kati, kufanya utafiti wa
masoko na bei za almasi na madini ya vito, kutunza takwimu za uzalishaji
na mauzo ya almasi na madini ya vito na
kusimamia tasnia ya almasi na madini ya vito nchini.
Kitengo cha TANSORT
kilianzishwa mwaka 1966 malengo yake yakiwa ni pamoja na kusimamia mrabaha
stahiki unaokusanywa na kulipwa serikalini na kuhakikisha madini ya almasi na
vito yanayozalishwa nchini yanapata bei
bora.
Imetolewa na:
WIZARA
YA NISHATI NA MADINI
12
Agosti, 2014
Post a Comment