
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (Kushoto) akizungumza na
Mwanaharakati wa Kimataifa wa haki za wanawake na watoto, Graca Machel
katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.Waziri Chikawe
alimueleza Mama Machel, juhudi zake za kuingiza katika Katiba Mpya
kifungu cha kuzuia mtoto wa chini ya miaka 18 asioe wala asiolewe.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akiagana na
Mwanaharakati wa Kimataifa wa haki za wanawake na watoto, Graca Machel
baada ya kikao chao kifupi kilichofanyika katika Hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam leo. Waziri Chikawe alimueleza Mama Machel, juhudi zake
za kuingiza katika Katiba Mpya kifungu cha kuzuia mtoto wa chini ya
miaka 18 asioe wala asiolewe.
WAZIRI wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe amekutana na Mwanaharakati wa
Kimataifa wa haki za wanawake na watoto, Graca Machel na kujadili
masuala mbalimbali ya haki za wanawake na watoto katika Hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam leo.
Katika
mazungumzo yao, Waziri Chikawe alimwambia mke huyo wa Rais wa zamani wa
Afrika Kusini, Nelson Mandela, juhudi zake za kuingiza katika Katiba
Mpya kifungu cha kuzuia mtoto wa chini ya miaka 18 asioe wala asiolewe.
Hata
hivyo, Mama Machel kwa upande wake alimshukuru Waziri Chikawe kwa maoni
yake na kusema kuwa ni muhimu kwa wadau wote wa haki za watoto
wakashinikiza wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba na watunga sheria wote
wahakikishe kipengele hicho kinaingia ndani ya Katiba.
Mama Machel yupo nchini kuhudhuria mkutano wa ufunguzi wa Kampeni ya Kitaifa ya kutokomeza ndoa za utotoni.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.



Post a Comment