Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ANYONGWA NA KUTUPWA KORONGONI HUKO KIGOMA!


 

Baba mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Kaga mkazi wa Mwanga Kisangani ''B'' jirani na Saigoni amemuua mpenzi wake kwa kumnyonga na kumtumpa katika makorongo ya Kilimahewa ''B'' Chini ya Shule ya Msingi Kilimahewa.


Taarifa za awali zinasema kulikuwa na ugomvi baina yao hao wapenzi wawili hali iliyopelekea mwanamke (Mama Koku) kumshtaki mwanaume mahakamani na kusababisha Mwanaume kufungwa miezi miwili jela. Siku kadhaaa baada ya mwanaume kutoka gerezani alipata habari kuwa mpenzi wake huyo aliyesababisha kuwekwa ndani anataembea na mwanaume mwingine ndipo mwanaume huyo alipopanga njama/namna ya kutekeleza mauwaji hayo.

Taarifa zinasema mara baada ya mwanaume kudhamiria kutekeleza tukio hilo lililo kinyume na neno la MUNGU katika kitabu kile cha Kutoka 20.13 alimwambia mpenzi wake kuwa; "Leo nimejisikia tutoke out twende Beach za Gorden tukajivinjari"  Mwanamke (Mama Koku) bila shaka lolote aliongozana nae mpenzi wake huyo ndipo wakiwa njiani katika makorongo ya Kilimahewa ''B'' mwanaume alimbadilikia ghafla na kumkaba kooni mwanamke na kupelekea kupoteza maisha. 
Mara baada ya mwaume kufanya unyama huo inasemekana zilipita siku kadhaa ndipo mwanaume alipowapiga simu kwa ndugu wa mwanamke huyo; "Njooni mchukue mzoga wenu!" Aliongea mwanaume huyo.

Mwanaume huyo anajishughulisha na shughuli za ubebaji mizigo katika soko kuu la Kigoma Mjini. 

Mara baada ya mwanaume huyo muuwaji kutoa taarifa kwa ndugu wa marehemu,ndugu walifanya jitihada za kumtafuta ndugu yao ndipo walipoukuta mwili katika Makorongo ya Kilimahewa ukiwa umeharibika vibaya na walilazimika kuzika hapo hapo.
Jeshi la Polis mkoani Kigoma linaendelea kumtafuta mtuhumiwa na atakapopatikana atapelekwa katika vyombo vya sheria.
Taarifa hii imethibitishwa na Diwani wa kata ya Mwanga Kaskazini Mh.Fransic Mangapi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top