Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Dodoma nako Hali Haikuwa nzuri.....Baadhi ya barabara zilifungwa kwa Muda


 

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi wa Polisi EMMANUEL G. LUKULA (ACP) akiongea na waandishi wa habari.

*******
Polisi  Mkoani  Dodoma JANA  asubuhi  ililazimika  kuzifunga  baadhi  ya  barabara  za  mkoa  huo  ili  kukabiliana  na  waandamanaji  wa  CHADEMA  waliokuwa  wamepanga  kuvamia  Bunge  Maalum  la  katiba  wakitaka  Lisitishwe.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi wa Polisi EMMANUEL G. LUKULA (ACP) amesema katika hilo kuna gari lenye namba za usajili T.792 CAX aina ya Pick up Ford Ranger nyeupe mali ya CHADEMA iliyokuwa ikiendeshwa na CHRISTOPHER NYAMWINJA, Mweneye miaka 52, Mgogo, Mkristo Mratibu wa CHADEMA Kanda ya magharibi ambapo makazi yake ni TABORA mjini limekamatwa mtaa wa KUU karibu na kituo cha mafuta cha GAPCO jirani na WIMPI RESTAURANT likiwa na watu wengine watatu ambao ni:-
  1. LAURENT S/O MANGWESHI mwenye miaka 36, Mkristo, Msukuma Mkulima wa Wialya ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
  2. AGNES D/O STEPHANO mwenye miaka 26, Mhehe, Mkristo Mfanyabiashara Mkazi Ubungo Maziwa Dar es Salaam.
  3. ELISHA S/O DAUDI mwenye miaka 49, Msukuma, Mkristo Fundi umeme Mkazi wa TAbora.
Kamanda LUKULA – ACP amesema gari hilo lilikuwa na bango lenye maandishi “TUNAPINGA UFISADI UNAOFANYWA NA BUNGE LA KATIBA”. Likiwa na maandishi ubavuni mbele na nyuma M4C.

Aidha Kamanda LUKULA – ACP ameongeza kuwa kabla ya kukamatwa kwa gari hilo Polisi walilikimbiza na katika kupita kwenye kona/mtaa watu wawili waliruka kutoka kwenye gari hilo na kukimbia kusikojulikana na bango hilo. Watu waliobaki ndani ya gari hilo ambao ni wanne ndio waliokamatwa.


Askari Polisi wakiwa katika ulinzi kudhibiti maandamano.

Jeshi la polisi limeimalisha ulinzi katika maeneo yote ambayo yalitajwa na chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa ndiyo watapitia wakiandamana kwenda kwenda Bungeni kuanzia saa 4 asubuhi ya JANA.
Polisi wakiwa wamefunga kamba kati barabara ya mzunguko ya stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani na chuo cha biashara CBE  kwaajili ya kuwazuia waandamanaji hao waliopanga kwenda Bungeni.


 Polisi wapanda farasi wakiimalisha ulinzi katika viwanja vya nyerere Squere ambapo Chadema wamepanga kuanzia maandamano kuelekea bungeni.
 Askali polisi wakiwafanya mawasiliano kwenye gari lao ambalo lilikuwa limepakia mbwa kwa ajili ya kuimalisha ulinzi katika viwanja vya Nyerere Dodoma kwa ajili ya kuwazuia waandamanaji wa Chadema walipanga kuandamana kwenda Bungeni.


Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top