STAA wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael 'Lulu' amemfagilia mama yake mzazi Lucresia Karugila kwa kupitia akaunti yake ya Instagram.
Lulu akiwa katika pozi na mama yake.
Staa
huyo ameachia picha yake wakati akiwa mdogo pamoja na mama yake kisha
kuandika ujumbe wa kumfagilia mama huyo ambao ulisomeka hivi:
Ni
miaka 19 sasa tangu tulipoanza rasmi mahusiano haya, ni mahusiano
ambayo yamekuwa na changamoto nyingi zaidi kwako kuliko kwangu. Ni mahusiano yanayomiliki mapenzi ya kweli na mapenzi yasiyo na usaliti.
Haijalishi
ni mara ngapi niliwahi kukukwaza na kukuumiza lakini hujawahi kuniacha
katika hali yoyote na kusema utafute mwingine wa kuwa naye.
Haijalishi ni wangapi wazuri umewahi kuwaona duniani lakini siku zote mimi ni mzuri zaidi katika macho yako.
Haijalishi
ni mabaya mangapi unayajua kuhusu mimi lakini unanitunzia siri zote
zilizo mbaya na nzuri....wewe ni mtu pekee ninayeweza kusimama duniani
na kujivunia kuwa ni wangu peke yangu, unayenipenda kiukweli, huwezi
kunisaliti wala kumuona yeyote mwingine bora zaidi yangu hata kama ikiwa
kweli..! Nakuombea afya, furaha, nguvu na siku nyingi za kuishi duniani...! NAKUPENDA MAMA!
Picha aliyoweka Lulu Instagram akiwa na mama yake enzi hizo
Post a Comment