Washiriki
wa shindano la dance 100% wa kundi la”Wakali sisi” Buguruni jijini Dar
es Salaam,wakionesha umahiri wao wa kudansi wakati wa mchuano wa nusu
fainali ya shindano hilo lililoandaliwa na EATV na kudhaminiwa na
Vodacom Tanzania lililofanyika kwenye viwanja vya Don Bosco
Oysterbay,Makundi 5 kati ya 10 yameingia fainali itakayofanyika mwezi
ujao.
Meneja
Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu,akikausha maji ya
mvua iliyokuwa ikinyesha kwa wingi wakati shindano la nusu fainali ya
Dance 100% na kusababisha shindano hilo kusimama mara kwa mara,Makundi 5
kati ya 10 yaliingia fainali itakayofanyika mwezi ujayo.Shindano hilo
lililoandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania lilifanyika
kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay.
Washiriki
wa shindano la dance 100% wa kundi la ”The Winners Crew” la jijini Dar
es Salaam,wakionesha umahiri wao wa kudansi wakati wa mchuano wa nusu
fainali ya shindano hilo lililoandaliwa na EATV na kudhaminiwa na
Vodacom Tanzania lililofanyika kwenye viwanja vya Don Bosco
Oysterbay,Makundi 5 kati ya 10 yameingia fainali itakayofanyika mwezi
ujao.
Kundi
la ”Mazabe Powder ” la Tegeta jijini Dar es Salaam,wakikonga nyoyo za
mashabiki wakati wa mchuano wa nusu fainali ya shindano la dance 100%
hapo jana lililoandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania
lililofanyika kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay,Makundi 5 kati ya
10 yameingia fainali itakayofanyika mwezi ujao.
Mmoja
wa washiriki wa Shindano la Dance 100% wa Kundi la “Quality Boys” la
Kinondoni jijini Dar es Salaam,akiwaongoza wenzake wakati wa mchuano wa
nusu fainali ya shindano la dance 100% hapo jana lililoandaliwa na EATV
na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania lililofanyika kwenye viwanja vya
Don Bosco Oysterbay,Makundi 5 kati ya 10 yameingia fainali
itakayofanyika mwezi ujao.
Wapenzi
wa shindano la Dance 100% wakisubiria kwa shindano hilo kuendelea mara
baada ya kusimama kwa muda kutokana na mvua iliyokuwa ikinyesha kwa
wingi wakati shindano la nusu fainali na kusababisha shindano hilo
kusimama mara kwa mara,Makundi 5 kati ya 10 yaliingia fainali
itakayofanyika mwezi ujayo.Shindano hilo lililoandaliwa na EATV na
kudhaminiwa na Vodacom Tanzania lilifanyika kwenye viwanja vya Don Bosco
Oysterbay.
SAFARI
ya shindano la Dance 100% imefikia patamu ambapo hapo jana makundi
matano kati ya makundi kumi yaliyochuana vikali katika nusu fainali ya
shindano hilo kwenye uwanja wa Don Bosco Oysterbay jijini Dar es
Salaam.Shindano hilo linaloandaliwa na kituo cha televisheni cha East
Africa(EATV) na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania limeleta mapinduzi
makubwa katika tasnia hii na kuweza kuwavutia vijana wengi kushiriki.
Makundi
ya wachezaji wa miondoko mbalimbali ya muziki ambayo yamefanikiwa
kuingia katika kinyang’anyiro hicho cha fainali ni Wazawa Crew,Best Boys
Crew,The W.T,Wakali sisi na The winners Crew.
Mratibu
wa mashindano hayo,Happy Shame,alisema kuwa katika kinyang’anyiro cha
nusu fainali hiyo wamefanikiwa kupata makundi 5 yatakayoingia moja kwa
moja kwenye fainali itayofanyika hapo baadaye.
“Huu
ni mwaka wa tatu EATV tunaandaa mashindano haya chini ya udhamini wa
Vodacom Tanzania mwaka huu mashindano haya yamekuwa na umaarufu mkubwa
na ushindani wa hali ya juu na kuwavutia vijana wengi ambao hujitokeza
kushiriki”Alisema Shame.
Shame,
aliongeza kuwa kundi litakaloibuka na ushindi katika mashindano haya
ambayo pia yamekuwa yakioneshwa na kituo cha EATV kila jumatano saa
moja kamili usiku,litajishindia kitita cha shilingi Milioni 5.
Naye
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa
shindano hilo,Matina Nkurlu aliwapongeza vijana wote walioshiriki katika
shindano hilo na kuwapa moyo wale ambao hawakufanikiwa kuingia fainali
kuwa wasife moyo kwani asiyekubali kushindwa si mshindani bali wajipange
upya na wawe wabunifu zaidi na kuweza kushiriki tena hapo mwakani.
Alisema
kuwa Vodacom inatambua kuwa jukumu la kukabiliana na tatizo la ajira
hapa nchini sio la serikali peke yake bali pia ni la watu wote ikiwemo
makampuni,taasisi za umma na za binafsi na ndio maana siku zote imekuwa
mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za kupambana na tatizo la
ajira kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo michezo , burudani na huduma
mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo kwani muziki na michezo ni
maeneo ambao yanaweza kutoa ajira kwa vijana na kuweza kuwakwamua
kimaisha.
“Vodacom
tunaamini kuwa vijana wanaweza kuleta mapinduzi makubwa katika sekta
mbalimbali iwapo watawezeshwa,hivyo tunadhamini mashindano haya
tukiamini kuwa vijana wenye vipaji wanaoshiriki wataweza kujitangaza na
kujulikana ambapo katika siku za usoni ni rahisi kujiajiri kupitia
katika sanaa”Anasema Nkurlu.
Pia
alitoa wito kwa wakazi wa jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi
katika fainali ya shindano hilo itakayofanyika hivi karibuni kuweza
kuwatia moyo vijana watakaotoa burudani kali na pia kununua bidhaa
mbalimbali za Vodacom zitakazopatikana kwa bei nafuu kabisa katika
shindano hilo kama vile Modem na Simu aina ya Samsung E1205 zote
zikiuzwa kwa shilingi 25,000 tu”Alisisitiza Nkurlu.
Post a Comment