Katika hali isiyokuwa ya kawaida watoto watatu wa familia moja
wameteketea kwa moto hadi kuwa majivu huku mmoja akibaki kichwa tu baada
ya nyumba waliyokuwa wamelala kuteketezwa kwa moto katika mtaa wa
Nyankumbu mjini Geita.
Akisimulia mkasa huo Baba wa familia hiyo Robert Reginald amewataja
watoto wake waliokufa kuwa ni Dimijius (4), Sofia (6), Reginald Robert
(8) ambaye kichwa chake pekee ndicho kilichobaki huku wengine viugo vyao
vikibaki kama mkaa.
Wathirika wengine ni mwanae Scholastika (16) ambaye yeye akipelekwa
katika hospitali ya rufaa Bugando alikokuwa amelazwa (ICU) na mkewe
aliyemtaja kwa jina la Angelina Gasper yeye ameungua vibaya mkono wa
kulia ambaye hali yake ikielezwa kuwa ni mbaya.
Haya ni mabaki ya vitu vilivyoungua ndani ya nyumba hiyo,wakiwemo kuku kama inavyoonekana katika picha
Haya ndio makaburi matatu ambapo miili ya watoto watatu imezikwa
CHANZO:FIKRAPEVU
Post a Comment