Mtuhumiwa katika kesi ya ugaidi, Abdallah Maginga, ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kumruhusu kutohudhuria siku za kesi na abaki magereza, kutokana na maumivu makali anayodai anayapata sehemu za siri alikominywa na polisi na kuingiziwa mti kwenye haja kubwa.
“Mheshimiwa
Hakimu naomba mahakama yako inipe ruhusa ya kutohudhuria siku ya kesi,
sababu ninapopanda gari napata maumivu makali sana sehemu za siri
kunauma kwa sababu polisi walinitesa kwa kuniingizia mti kwenye haja
kubwa na kuminya sehemu zangu za siri,” alisema.
Alisema
mbele ya Wakili wa Serikali, Rose Sulle kuwa mbali na maumivu ya sehemu
za siri, pia mguu wake uliokatwa hospitalini, bado unamsumbua kutokana
na maumivu.
Maginga
pia aliomba iagize Magereza wamruhusu akatibiwe hospitalini, kwani
alitakiwa kwenda kupata matibabu Septemba 5 mwaka huu, ila alizuiwa hadi
sasa.
Akijibu
hoja hizo, Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo, Devotha Msofe, alisema
suala la kuja mahakamani ni lazima na mahakama haiwezi kumpa ruhusa
hiyo.
Pia,
alimshauri mshitakiwa huyo kuwa kama ana maelezo mengi, amweleze hakimu
anayesikiliza kesi yake, Mustapher Siyani ambaye kwa siku hiyo
hakuwepo.
“Sikiliza
Maginga suala la kuja mahakamani ni lazima na sio hiyari wala
majadiliano, ila kuhusu kwenda hospitalini liwasilishe Magereza ndio
mtaona kwa pamoja mnafanyaje,” alisema.
Awali
ilidaiwa mahakamani hapo kuwa washitakiwa hao wameshitakiwa kwa makosa
yaliyo chini ya Sheria ya Kuzuia ugaidi, ambapo Sheria Namba 22 ya
Mwaka 2002 inasema upelelezi ukishakamilika, Mahakama Kuu ndiyo yenye
mamlaka ya kuisikiliza na kutoa uamuzi.
Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka ya kuua, kujaribu kuua, kusajili na kusafirisha vijana kujiunga na Al-Shabaab.
Mbali
na mashitaka hayo, pia wanahusishwa na tukio la mlipuko wa bomu
lilitokea baa ya Arusha Night Park jijini Arusha na kusababisha kifo
cha mtu mmoja na kujeruhi wengine 16.
Watuhumiwa
wengine wanaokabiliwa na mashitaka hayo ni Abdallah Athumani, Abdallah
Thabiti, Ally Hamisi, Abdallah Wambura, Rajab Hemedi, Hassan Saidi, Ally
Hamisi, Yassin Sanga, Shaaban Wawa, Swaleh Hamisi, Abdallah Yassin,
Abdallah Maginga na Sudi Nassib Lusuma.
Wengine
walioongezwa katika shauri hilo ni Shaaban Mussa, Athuman Hussein,
Mohammed Nuru, Jafari Lema, Abdul Mohammed na Said Michael Temba.
Post a Comment