Machi mwaka jana, Faraji alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela au faini ya zaidi
ya Sh. milioni 200 baada ya kupatikana na hatia ya kutakatisha fedha
haramu kwenye Benki ya NBC, Tawi la Dar ambapo jamaa huyo alishindwa
kulipa kiasi hicho cha fedha na kujikuta ‘akiozea’ Segerea au Segedansi
kama wanavyoita mastaa wa Kibongo.
UTAJIRI WA GHAFLA
Katika
msala huo, Kajala alihukumiwa miaka mitano jela au faini ya Sh. milioni
13 kwa kukutwa na hatia ya kuuza nyumba yao iliyowekwa kizuizini na Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ambapo alilipiwa shilingi
Milioni 13 na Wema Isaac Sepetu na sasa anapeta mtaani na utajiri wa
ghafla.
HOJA YA MSINGI
Baada ya
kuokolewa jela na Wema, Kajala ametembelewa na utajiri ambapo amekuwa
akitanua mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar, akisukuma magari ya kifahari,
kupanga ghorofa maeneo ya Sinza-Madukani anayolipia Sh. milioni 3.2 kwa
mwezi, akimiliki kampuni ya kuzalisha sinema ya Kay
Entertainment huku akaunti yake ikiwa imenona kwa mamilioni kadhaa.
GEREZANI SEGEREA
Hivi karibuni, ‘mtu wetu’ alikwenda kumtembelea Faraji kwenye Gereza la Segerea, Dar ambapo alipata nafasi ya kutoa la moyoni juu ya mkewe Kajala ambaye alifunga naye ndoa kanisani miezi michache kabla ya kukutwa na msala huo.


Post a Comment