MECHI
ya Ngao ya Jamii kuashiria kufunguliwa kwa pazia la ligi kuu soka
Tanzania bara msimu wa 2013/2014 baina ya mabingwa Azam fc na makamu
bingwa, Dar Young Africans sasa utapigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam septemba 14 badala ya septemba 13 mwaka huu kama ilivyopanga.
Shirikisho
la soka Tanzania limeamua kuusogeza kwa siku moja mchezo huo uliotakiwa
kupigwa jumamosi na sasa kupigwa jumapili kwa lengo la kuwapa fursa
mashabiki wengi kuuona.
TFF
imesema jumapili ni siku tulivu kuliko jumamosi na mchezo wa mwaka huu
utaambatana na shughuli za kijamii ikiwemo uchangiaji wa damu.
Pia sehemu ya mapato ya mchezo huo yatapelekwa katika shughuli ya kijamii iliyochaguliwa.
Mechi
hiyo itapigwa ikiwa ni wiki moja kabla ya kuanza kwa ligi kuu septemba
20 mwaka huu ambapo Yanga wataanzia ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar katika
dimba la Jamhuri mkoani Morogoro.
Mnyama
Simba atakuwa uwanja wa Taifa siku moja baada ya kufunguliwa kwa ligi
kuu (septemba 21 mwaka huuu) dhidi ya Wagosi wa Kaya, Coastal Union.
Azam fc watakuwa nyumbani Azam Conmplex kuchuana na Polisi Morogoro.


Post a Comment