Mjumbe
wa Bunge Maalum, Mhe. Prof. Mark Mwandosya akichangia mjadala wa ndani
ya Bunge Maalum kujadili taarifa za kamati za bunge hilo
zilizowasilishwa wiki iliyopita kwa ajili ya kuandika Katiba
inayopendekezwa.(Picha na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)
Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
MJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Prof. Mark
Mwandosya ameeleza kuwa mpaka ifikapo mwaka 2055 Tanzania itakuwa imeachana na
umaskini katika nchi ya uchumi wa kwanza endapo kutakuwa na dhamira ya dhati hususani
kuwa kuandika Katiba yenye kuleta nafuu kwa watanzania kwani kila kitu kwa
Waafrika kinawezekana pasipo kuwa na Wazungu.
Prof. Mwandosya alisema hayo jana wakati akichangia
mjadala wa katiba ndani ya Bunge Maalum, ambapo alisisitiza umuhimu wa kuwa na
katiba itakayozingatia vipaumbele ambavyo vinaweza kumkwamua mwananchi wa
kawaida kuondokana na umasikini na kuliinua Taifa kiuchumi.
Mhe. Mwandosya amesema kuwa kuhusu changamoto na kero
zinazohusu mambo ya Muungano, katiba imejaribu kuzizingatia karibia zote, huku
akieleza kuwa hali ya Muungano ni imara na itaendelea kuwa imara.
Ili kufanikisha nchi inapiga hatua baada ya kuwa na
Katiba bora, Mhe. Mwandosya amefafanua kuwa, watumishi wote wa Umma hawana budi
kuliletea tija Taifa hili kwa kuwa misingi imewekwa ndani ya rasimu ya
katiba na kusisitiza kuwa Mtumishi wa
Umma sio mtawala na mambo yanayohusu miiko na maadili ya mtumishi huyo yenye
kumtumikia mwananchi serikali Katiba imeweza kuyazungumzia.
“Tumezungumzia kuhusu rushwa ambaye ni adui wa haki,
kwamba hili tulitambue katika Katiba ili katika Sheria likasimamiwe vilivyo na
pia tumezungumzia pia wale wanaouhujumu uchumi”, alisema Mhe. Mwandosya.
Kuhusu haki za vijana, Mhe. Mwandosya ameeleza kuwa
katika Rasimu ya Katiba wamezungumzia juu ya haki za vijana, haki za walemavu,
haki za wazee, pamoja na haki za watoto, huku akiwashangaa baadhi ya wajumbe
walioko nje ya bunge hilo wanapotoa shutuma kuwa wanapoteza wakati kana kwamba
hawazungumzii mambo yanayowahusu wananchi.
“Nawaomba wananchi watusikilize na wayazingatie haya
tunayoyasema”. Alisema Mhe. Mwandosya.
Akizungumzia kuhusu Vyombo vya Usalama, amesema kuwa
Katiba inawalinda na kuwatambua viongozi wa usalama, ambapo sheria inawapa haki
hata baada ya kustaafu ili wakaweze kuishi maisha bora kwa kuchukua dhamana
kubwa, hivyo kwa dhamana hiyo viongozi hao wanapostaafu wanatakiwa kujiepusha
na masuala ya kisiasa kwasababu.
“Usalama wa Taifa, Jeshi, Polisi, Magereza na
Uhamiaji, hawa tunawatengezea mambo mazuri sana wanapostaafu, kwahiyo tafadhari
sana mkishatoka tusaidieni, toeni ushauri lakini mkijiingiza katika siasa na
mafaili yetu huku mmeyashika hamtutendei haki”, alisema Mhe. Mwandosya.
Aidha, ameomba kuwepo na Randama kwani hiyo inaandikwa
katika lugha ambayo mwananchi anaweza kuisoma tofauti na katiba kwani hiyo
inaandikwa kwa lugha ya kisheria, kwahiyo amependekezo kuwepo na randama kwa
ajili ya wananchi.
Mwandosya ameongezea juu ya suala la amani kuwa ni
jambo kubwa sana, amewananga watu wenye tabia ya kutaka wananchi kuandamana
wakapigwe risasi hao ni watu wasioitakia mema nchi, hivyo amewaasa wananchi
walipinge kwa nguvu zao zote kuhusu suala hilo.
“Nina ushauri kwa viongozi wenye kutaka wananchi
wakapigwe risasi na Polisi, naomba watangulie wao wajipige risasi, unapotaka
kuwa Shujaa anzia kwanza wewe mwenyewe, usiwapeleke vijana ambao ni matumaini
ya nchi yetu, ndugu zangu hili jambo siyo la busara hata kidogo na wananchi
mnapokwenda kuandamana, vijana mseme mnaandamana kwa nini? Kwasababu gani? Na
kwa misingi gani na kwasababu ya nani? Ukishajibu haya maswali kwakweli mtaona
nchi yetu kuwa ni nzuri sana, nchji ya amani”, alisisitiza Mhe. Mwandosya.
Post a Comment