Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RAIS KIKWETE ZIARANI NCHINI MAREKANI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete ameondoka nchini usiku wa jana, Jumatatu, Septemba 15, 2014, kuanza  ziara ya wiki mbili katika Marekani ambapo atahutubia Mkutano wa 69 wa Baraza  Kuu la Umoja wa Mataifa (UN General Assembly) New York.
Mbali na kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, 
Rais Kikwete pia atahudhuria mikutano muhimu katika mji mkuu wa Marekani, Washington, D.C.
Mjini New York, Rais Kikwete atashiriki katika mikutano mikubwa zaidi ya
10 ikiwa ni pamoja na kuhutubia Baraza Kuu wakati wa Majadiliano ya Jumla ( General Debate) yaliyopangwa kufanyika Septemba 24 hadi 27 na Septemba 29 hadi Oktoba Mosi, mwaka huu, 2014.
Rais Kikwete amepangwa kuwa kiongozi wa 12 duniani kuhutubia Baraza
hilo mchana wa Alhamisi ijayo, Septemba 25, 2014. Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utaanza Septemba 16 hadi Desemba 24, mwaka huu, Miongoni mwa mikutano mingine muhimu ambayo Rais Kikwete atashiriki ni pamoja na kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) Kuhusu Mazingira (CAHOSC) na Mkutano wa Wakuu wa Nchi Kuhusu Mazingira ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN),  Mheshimiwa Ban Ki Moon.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
16 Septemba , 2014.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top