Emmanuel Okwi
REKODI
zinaonyesha kwamba Simba haijawahi kushinda kesi ya kumwania mchezaji
yeyote kati yake na Yanga au Costal Union kwa takribani miaka 20.Mara
kadhaa timu hiyo yenye maskani yake Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini
Dar es Salaam imejikuta ikibwagwa katika vita ya kugombea mchezaji kati
yake na klabu hizo, lakini hukumu za wachezaji Emmanuel Okwi na Abdul
Banda zilizotolewa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF
Jumapili iliyopita kwa mara ya kwanza imewapa Simba ushindi dhidi ya
Yanga na Coastal Union.
Hapa chini ni baadhi ya wachezaji ambao wamewahi kugombewa na timu hizo dhidi ya Simba.
Mtemi Ramadhani Mwaka 1980;
Simba
ilimgombea kiungo huyo na Yanga. Mchezaji huyo alikuwa akichezea Waziri
Mkuu ya Dodoma lakini alijikuta akisajili katika timu za Simba na
Yanga.
Akiwa
na Taifa Stars iliyokuwa imekwenda Nigeria kucheza Fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika (Afcon), Mtemi alizua balaa Uwanja wa Ndege wa Dar es
Salaam wakati Stars walipokuwa wakirejea.
Viongozi
wa Simba na Yanga na wale Pan African walikuwa kiwanjani hapo kuwalinda
wachezaji waliowasajili na kuwafanya washikane mashati.
Mbali na Mtemi,Yanga pia walikuwa wakimgombea, Rashid Idd ‘Chama’ waliokuwa wamemsajili wao pamoja na Pan African.
Chama
cha Mpira wa Miguu (FAT, sasa TFF), chini ya Mwenyekiti wake, Said El
Maamry waliwawataka wachezaji hao kuchagua timu za kuchezea.Mtemi
alichagua kuchezea Simba na Chama aliichagua Pan African lakini Yanga
hawakukubali wakakata rufaa Baraza la Michezo Tanzania (BMT).
BMT
iliamua kuwafungia wachezaji hao kwa mwaka mmoja, baada ya hapo Mtemi
alirudi Waziri Mkuu na baada ya msimu mmoja akajiunga na Simba. Chama
naye aliendelea kuchezea Pan African.
Yussuf Bana; Mwaka 1981
Simba
ilimgombea beki Yussuf Ismail Bana katika vita na Yanga. Beki huyo
alicheza Simba msimu mmoja tu na kuamua kujiunga na Yanga mwaka 1982
kitu kilichozua utata mkubwa. Inadaiwa, Yanga ilimsajili kwa jina lake
halisi la Yussuf Ismail na Simba walimsajili kwa jina la Yussuf Bana
ambalo lilidaiwa kuwa ni jina la la utani.
Baada ya vita ya chinichini hatimaye, Bana ambaye kwa sasa ni marehemu aliruhusiwa kuchezea Yanga.
Francis ’Fura’ Mwikalo;
Simba
ilipoteza matumaini ya kunyakuwa ubingwa wa Tanzania Bara mwaka
1985/86 baada ya kumsajili mchezaji wa zamani wa Coastal Union ya Tanga,
Francis Mwikalo.
Katika
kutaka kuonyesha kwamba mchezaji huyo alikuwa ni tofauti na Mwikalo wa
Coastal Union, Simba walimbadilisha jina na kumsajili kwa jina la Fura
Mwikalo.
Sakata
la mchezaji huyo lilikuwa kubwa sana na kufikia hatua ya kuamuliwa na
Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu jijini Dar es Salaam. Siku ya hukumu,
mashabiki, wapenzi na wanachama wa Simba walifika mahakamani wakiwa
na ngoma ya Kizaramo aina ya Mdundiko wakiamini kwamba watashinda kesi
hiyo na kutangazwa kuwa mabingwa.
Baada
ya hukumu kutolewa na Simba ilibwagwa na kupoteza pointi zote
walizomchezesha Mwikalo ambaye awali walidai kuwa walimsajili kutoka
Muheza Shooting ya Tanga.
Athuman Idd ‘Chuji’;
Yanga
iliiwaduwaza tena watani zao kwa kumnyakuwa beki wa zamani wa Polisi
Dodoma, Athumani Idd Chuji ambaye aliikacha Simba katika hatua za mwisho
mwaka 2006.
Pamoja
na Mwenyekiti wa Simba wakati huo, Hassan Dalali kudai kwamba Chuji
hatacheza soka, mchezaji huyo alisema ni heri akauze ndimu kuliko kurudi
Simba. TFF ilimwidhisha kuchezea Yanga.
Mbuyu Twite;
Agosti,
2012 aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage alisafiri kwenda
DR Congo kumsajili beki Mbuyu Twite. Hata hivyo, Yanga waliwazidi akili
na kumsajili beki kwa kile kilichoelezwa kwamba Simba walishindwa
kufuata sheria za usajili.
Simba ilidaiwa kukurupuka bila ya kufuata sheria za CAF na Fifa, hivyo TFF kumwidhinisha kuchezea Yanga.
Kelvin Yondani;
Mwaka huohuo, Simba ilipata pigo lingine kubwa baada ya beki wake wa kati Kelvin Yondani kusajiliwa na Yanga.
Awali, Yondani aliondoka Simba na kwenda kujichimbia Mwanza ambako alipoibuka alitua Jangwani kwa dau la Sh30 milioni.
Pamoja Rage kudai kwamba Yondani asingeweza kucheza soka TFF ilimwidhinisha mchezaji huyo kukipiga Yanga.
Mrisho Ngassa;
Baada
ya kumchukua kwa mkopo kutoka Azam, Simba walimwongezea Ngassa usajili
wa mwaka mmoja na kumpa gari pamoja na Sh25 milioni.
Msimu
wa kutolewa kwa mkopo Simba ulipoisha, Yanga ilimsajili Ngassa kwa ada
ya Dola 30,000.Simba hawakukubali, lakini TFF ilimwidhinisha Ngassa
kuchezea Yanga na kumtaka kurudisha fedha za Simba alizopewa,
piaalifungiwa michezo sita.
Iliwabidi Simba kusubiri hadi Jumapili iliyopita kuibadili kibao
Post a Comment