JESHI la
polisi mkoa Kigoma limefanikiwa kukamata silaha za kivita aina ya SMG, mabomu
matatu ya kutupa kwa mkono, risasi 64 pamoja na kuwauwa watu watano
wanaosadiliwa kuwa ni majambazi wakati wa purukushani za majibizano baina
majambazi hao na askari polisi mkoani Kigoma.
Akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari mkoani humo kamishina msaidizi wa polisi mkoa
kamanda Japhal Ibrahim alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 11:45
alfajiri Septemba 3 mwaka huu, katika barabara kuu ya Kasulu – Kibondo eneo la
pori la Malagalasi Wilayani Kasulu.
Kwa mujibu
wa kamanda Ibrahim alisema askari polisi wakiwa katika doria walipata taarifa
za majambazi kutoka nchi jirani ya Burundi wakitaka kufanya uhalifu wa
unyang’anyi wa kutumia silaha kuteka magari ya wasafiri yaliyokuwa yakipita
katika barabara hiyo.
Alisema
kufuatia taarifa hiyo askari polisi walijipanga na kuweka mtego katika eneo
lililokusudiwa kufanyika uhalifu huo ambapo baada ya muda watu hao walifika
eneo la tukio ili kukamilisha azma yao ambapo askari waliwafuata ndipo
walipoanza majibizano ya risasi na askari polisi.
Katika tukio
hilo askari walifanikiwa kuwauwa majambazi wote watano ambapo katika eneo la
tukio hilo walikuta mabomu matatu, silaha mbili za kivita aina ya SMG
No. 691220 pamoja na AK 47 no. UA40501997 magazini tatu zenye
risasi 64 sambamba na mikate na juice aina ya Zaam Zam orange kutoka katika
kampuni ya Monas Beverages.
Kamanda
alisema miili ya majambazi hao ipo katika hospitali ya wilaya ya Kasulu ambapo
majina yao hayajatambulika huku askari polisi waliokuwa katika tukio hilo
wakiwa wamesalimika na hakuna aliyejeruhiwa ambapo msako unaendelea katika
maeneo yote ili kukomesha vitendo vya uhalifu mkoani Kigoma.




Post a Comment