Mwanasoka
bora wa dunia Cristiano Ronaldo jana alizidi kuisogelea rekodi ya
ufungaji bora wa muda wa ligi ya ulaya inayoshikiliwa na Raul Gonzalez
Blanco.
Mpaka kufikia jana Raul Gonzalez alikuwa akiongoza listi ya wafungaj
bora wa muda wote wa ulaya akiwa na magoli 71, Ronaldo na Messi wakiwa
wamefungana wote wakiwa na magoli 68.
Lakini jana Ronaldo akiichezea klabu yake ya Real Madrid jana usiku
dhidi ya Ludogorets ya Bulgaria, alifunga goli lake la 69 katika
michuano ya ulaya na hivyo kumpita mpinzani wake Lionel Messi mwenye
magoli 68.
Mchezo wa jana uliisha kwa ushindi wa 2-1 kwa Real Madrid, Karim Benzema akifunga goli lingine la Madrid.
Angalia magoli hapa chini


Post a Comment