Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

FISI AFUNGA MITAA MJINI SINGIDA, WANANCHI WATIMUA MBIO NA KUTELEKEZA NYUMBA ZAO

 


Katika hali isiyo ya kawaida wakazi wa manispaa ya Singida wameingiwa na taharuki na kuanza kukimbia ovyo baada fisi kuonekakana  katikati ya mji wa Singida akiwa anakimbia na kuingia katika maduka ya wafanya biashara.

Wakieeleza  kwa hisia tofauti baadhi ya wakazi  huku wengine wakiwa wamepanda juu ya mapaa ya nyumba pamoja na watoto wao  kwa hofu ya kuumwa,wamesema kuonekana kwa fisi mjini katikati  ni jambo la ajabu kwani wanyama kama hao honekana vijiji au porini,wengine wamesema labda mnyama huyo amechelewa kurudi vichakani wakati alipokuwa amekuja kula mabaki ya chakula mjini. 
 
Akielezea tukio hilo Afisa maliasili mkoa wa Singida Bwana Charles Kidua amesema pamoja na kwamba wanyama kama fisi wapo katika manispaa ya Singida na pindi wanapo onekana katika maeneo ambayo siyo ya kawaida ,Basi wananchi watoe taarifa kwa mamlaka husika kwani wanyama kama haho  wana weza kuwa na ugonjwa wa kichaa ,badala ya kujichukulia hatua mkononi ya kuwaua.
 
Kutokana na umati wa wananchi kuwa wengi wakati wakimfukuza fisi huyo bila kujali askari waliokuwa wakituliza fujo huku wakiwa na silaha,wanachi walifanikiwa kuwapokonya askari fisi baada ya kumtega na kamba huku wakiimba tunataka fisi wetu na kuamua kumkimbiza mjini huku wakimpiga umbali wa kilomita mbili.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top