BAADA ya
tetesi kuzagaa kwamba aliyekuwa Katibu wa Bongo Movie Unity, William
Mtitu kwamba ana bifu kali na aliyekuwa mwenyekiti wa kundi hilo, Steven
Mengere ‘Steve Nyerere’ mwenyewe amefunguka kwamba hawezi kufanya kitu
kama hicho.Aliyekuwa Katibu wa Bongo Movie Unity, William Mtitu.
Akistorisha na paparazi wetu, Mtitu amesema anashangazwa na taarifa hizo
licha ya kwamba hawajawahi kuzungumza na Steve tangu alipoachia ngazi
ya ukatibu.
“Sijawahi kutishia kuua mtu kama watu wanavyosema, Steve ni mdogo
wangu hivyo kama atakuwa na bifu na mimi ni yeye na sitajali kwani
wangekuwa ni kina Ray au wasanii wengine wakubwa wamenichunia ningewaza
lakini huyo haniumizi kichwa,” alisema Mtitu.

Aliyekuwa mwenyekiti wa kundi hilo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Maddi yaliyopo mtaani ni kwamba, wasanii hawa kwa sasa ni kama paka na
panya na imefika hatua ya kutishiana kuuana.


Post a Comment