Jana
ndio Waziri mkuu mpya wa Uganda Ruhakana Rugunda kaapishwa ila kabla
yake alikua ni Amama Mbabazi ambae alifutwa kazi wiki kadhaa zilizopita
baada ya kukaa madarakani toka May 2011 akitokea kwenye Uwaziri wa
Ulinzi.
September 18 2014 ndio Rais Museveni alimuandikia Spika wa bunge
barua kumuarifu kuwa ameamua kumuondoa waziri mkuu huyo na nafasi yake
kuchukuliwa na aliyekua Waziri wa Afya ambae kwa sasa ana umri wa miaka
67.
waziri huyu alietimuliwa alikua Waziri mkuu
wa nne toka Rais Museveni aanze kuitawala nchi hiyo January 1986 ambapo
mpaka sasa amewahi kuwa na Makamu wa Rais wanaofikia wanne.
Picha zote hizi zinaonyesha wakati Serikali ya Uganda
ilipomnyang’anya ulinzi wa Wanajeshi waziri huyu mkuu baada ya kufutwa
kazi ambapo kwenye hii picha ya chini anaeonekana ni mke wake
akilalamika kwa kutoamini kilichotokea kwani mume wake na Rais Museveni
wamekua marafiki wakubwa.
Vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti kwamba kuna mambo mengi
yaliyosababisha kufutwa kazi kwa waziri huyu mkuu lakini mambo hayo
hayajawekwa wazi.
Nyuma hii unayoiona ni nyumba anayoishi na inayomilikiwa na Waziri huyu mkuu aliefutwa kazi.





Post a Comment