Mahakama
ya hakimu mkazi Kinondoni jijini Dar es Salaam imezuia kufanyika kwa
tamasha lililopewa jina ‘Bang Bang Bear Fest’ lililokuwa linatarajiwa
kufanyika Jumamosi hii.
Uamuzi
wa mahakama hiyo umetokana na malalamiko yaliyotolewa na Bongo5 Media
Group ambao wanamiliki wazo halisi la tamasha la aina hiyo liitwalo Dar
es Salaam Bear Fest.
Kwa
hali hiyo mahakama hiyo imetoa amri ya kusitishwa mara moja kwa ‘Bang
Bang Bear Fest’ lililokuwa lifanyike October 4 kwenye viwanja vya Posta
Kijitonyama, Dar es Salaam pamoja na kulipa hasara yoyote iliyotokana na
kuingiliwa kwa haki miliki hiyo.

.jpg)
.jpg)

Post a Comment