Wakati
mkataba wake wa mkopo ukiwa umebakisha miezi nane kuisha, usajili wa
Radamel Falcao kwenda Manchester United umechukua nafasi kwenye vyombo
vya habari vya Uingereza vinavyoripoti kwamba Man United imekubaliana
rasmi na mahitaji binafsi ya mchezaji huyo kwa ajili ya kukamilisha
usajili wa kudumu.Taarifa zinaeleza kwamba Man United wanafanya jitihada
zote kumaliza suala la usajili wa Falcao ili kuepuka kila kilichotokea
miaka mitano iliyopita katika usajili wa Carlos Tevez……. United
walimsajili Falcao kwa mkopo kutoka Monaco siku ya mwisho ya usajili wa
wakati wa kiangazi.
Wakiwa
tayari wameshalipa ada ya mkopo wa £6million kwa klabu ya Ufaransa,
United pia walishakubaliana kimsingi na Monaco kuwalipa kiasi cha £43.5m
ikiwa wataamua kumchukua Falcao kiujumla mwishoni mwa msimu.
Baada ya
hayo yote, leo imeripotiwa kwamba mkurugenzi mkuu wa United Ed Woodward
tayari amekubaliana na wawakilishi wa Falcao kumlipa mshahara wa
£250,000 kwa wiki mchezaji huyo pamoja na bonasi na haki za taswira yake
kutumika ambapo kwenye sentensi nyingine club hii imekanusha taarifa
kwamba itakatisha mkataba wa mkopo wa Falcao ikiwa mchezaji huyo ataumia
tena goti.



Post a Comment