Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Shibuda Anena...."Heri kuwa msaliti kuliko mhaini".....Ampongeza Rais Kikwete kwa usikuvu, Awapiga vijembe CHADEMA

 

 
MJUMBE wa Bunge Maalumu, John Shibuda, amesema ni heri kuwa msaliti kuliko kuwa mhaini kwa maslahi mapana ya Watanzania.
Shibuda ambaye alipewa nafasi kuzungumza baada ya Katiba Inayopendekezwa kupatikana, alisema anatoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), lakini amepinga kuwa sehemu ya kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Alisema anajua ataitwa msaliti, jambo alilosema ni vyema kuitwa hivyo kuliko kuwa mhaini wa maslahi ya Watanzania.
Alisema katika mchakato huo, Rais Jakaya Kikwete amewafundisha Watanzania kuwa ni msikivu kiasi cha kusikiliza uongo, huku akijua kuwa ni uongo lakini akaendelea kusikiliza.
Shibuda alisema utumishi wake ni kwa Watanzania na kamwe hauwezi kuwa kwa maslahi ya kikundi cha watu.
Kwa mujibu wake, Bunge Maalumu la Katiba, limeepuka watu ambao afya zao za ubongo zina mgogoro, ndio maana wakati wote wanawaza ufedhuli.
Aliwataka wananchi hao kuwa makini na makatazo ya dini, ambazo zimeasa kuja kwa zama za manabii wa uongo, ambao alisema siasa imegeuka mfereji wa manabii hao.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top