Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Bw. Jumanne Sagini akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) Daftari la Wapiga Kura linalotumika kuandikisha wananchi katika
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Kushoto ni Mratibu wa Uchaguzi huo Bw. Denis Bandisa.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini akiongea na waandishi wa
habari kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Desemba
14 mwaka huu ambapo amesema hadi sasa maandalizi yote yamekamilika. Kushoto ni
Mratibu wa Uchaguzi huo Bw. Denis Bandisa na kulia ni Afisa Mwandamizi wa
TAMISEMI Bw. Mohamed Mavura.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini akitoa wito kwa wananchi
kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye
Daftari la Wapiga Kura ili waweze kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali
za Mitaa mwaka huu. Pia Katibu Mkuu huyo amewataka Viongozi wote wanaosimamia
uchaguzi huo kuzingatia sheria na kanuni za uchaguzi. Kushoto ni Mratibu wa
Uchaguzi huo Bw. Denis Bandisa na kulia ni Afisa Mwandamizi wa TAMISEMI Bw.
Mohamed Mavura.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini akitoa wito kwa Viongozi wa Vyama vya Siasa,
Wagombea na Washabiki wao kuendesha kampeni kwa amani, utulivu na ustaarabu bila
kukiuka kanuni na taratibu zilizowekwa. Kushoto ni Mratibu wa Uchaguzi huo Bw.
Denis Bandisa.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw.
Jumanne Sagini akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) Kanuni za
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mwaka 2014 ambazo tayari zimesambazwa kwa
wadau wote wa uchaguzi huo. Aidha amesema kuwa Kanuni hizo zimewekwa katika
Tovuti ya TAMISEMI ambayo ni www.ps@pmoralg.go.tz . Kushoto ni Mratibu wa Uchaguzi huo Bw. Denis
Bandisa.
Mratibu
wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kutoka TAMISEMI Bw. Denis Bandisa akifafanua
utaratibu wa kumuandikisha Mpiga Kura katika Daftari laWapiga Kura wa Uchaguzi
wa Serikali za Mitaa. Amesema Serikali imetenga Shilingi Bilioni 20 kwa ajili
ya Uchaguzi huo. (PICHA
NA MAELEZO).
Post a Comment