Mtu mzima ovyoo! Akina
mama watatu ambao ni wake za watu, wanaounda Kundi la Heshima Pesa
Shikamoo Makelele lenye maskani yake maeneo ya Mawenzi mjini hapa
wanadaiwa kuwachefua baadhi ya watu baada ya kujitoa fahamu na kumwaga
‘lazi’ hadharani na mbaya zaidi mbele ya watoto wadogo.
Wake
za watu wanaofahamika kama mama Sabra mwenye kigauni kifupi cha
draftidrafti, mama Jenifa mwenye kimini cha njano na mama Athuman
wakijitoa ufahamu mbele ya mahrusi.
Kwa mujibu wa ‘shujaa’ wetu, tukio hilo la aibu ya aina yake lilijiri
juzikati kwenye Ukumbi wa Savoy mjini hapa ambapo wanawake hao
walialikwa kuburudisha kwenye sherehe ya harusi ya jirani yao.
Wanawake hao waliofahamika kwa majina ya watoto wao ni pamoja na mama
Sabra aliyekuwa akibinuka, aliyevalia kigauni kifupi cha
draftidrafti.Mwingine alikuwa ni mama Jenifa aliyekuwa ametupia kimini
cha njano na mama Athuman ambao kwa pamoja walikuwa na vikuku miguuni.
Mtu wetu huyo aliyekuwa ndani ya ukumbi huo aliwashuhudia wanawake hao
wakimwaga lazi mara baada ya MC kuita kundi lao kwa ajili ya kutoa
zawadi.
Kabla ya kutoa zawadi, wamama hao walimfuata DJ na kumtaka kuwawekea
wimbo wowote wa Taarab, wakawekewa ambapo wakiwa na zawadi yao ya doti
moja ya khanga, walipita mbele ya maharusi kwa mbwembwe zote na baada ya
kukabidhi zawadi hiyo ndipo balaa lilipoanza.
Huku wakipeana nafasi na mara nyingine kulaliana, walikuwa wakijibinua
na kuonesha staili za chumbani huku ‘makufuli’ yakiwa nje, jambo
lililotibua harusi hiyo.
Ilifika hatua hadi baadhi ya wazazi wakawa wanawaziba watoto wasione,
jambo lililosababisha wazazi wa pande zote mbili (wakwe) kununa pamoja
na MC wa shughuli hiyo, MC Chuma ambaye baada ya kuona wanawake hao
wanazidi kuvua nguo aliwashtua:
“Ninyi mnaofanya hivyo mjue OFM (Oparesheni Fichua Maovu ya Global
Publishers) ipo humu ndani, sasa kesho au keshokutwa msitafute lawama.”
Pamoja na angalizo hilo la MC, ndiyo kwanza wanawake hao walipozidi kumwaga lazi ikawa ni laana tupu.
Baada ya pati kukamilika, mwanahabari wetu aliwafuata wanawake hao na kuwahoji kulikoni kumwaga radhi kiasi hicho? Msikie huyu:
“Kazi yetu ni kuchangamsha sherehe. Shughuli ilipooza lakini baada ya
sisi kuserebuka, ilibadilika, habari ndiyo hiyo,” alisema mama Sabra.
Baada ya pati kukamilika, mwanahabari wetu aliwafuata wanawake hao na kuwahoji kulikoni kumwaga radhi kiasi hicho? Msikie huyu:


Post a Comment