
Rais wa nchi ya China, Xi Jinping akiwapa mkono wananchi wa Tanzania.
Inadaiwa
kuwa wanunuzi, raia wa Uchina walinunua maelfu ya kilo za pembe za
ndovu nchini Tanzania na kuzitorosha kutoka nchini humo katika ndege ya
binafsi ya Rais wa Uchina, Xi Jinping wakati alipozuru bara Afrika.
Kulingana na shirika la ujasusi la mazingira lililo na makao yake mjini
London.
Pembe
hizo zilinunuliwa wiki moja tu kabla ya ziara ya rais huyo wa China kuja
nchini tanzania mwaka ulioipita ambapo zilifichwa katika mifuko ya
wanadiplomasia ili kutokamatwa.
Shirika hilo pia linadai kwamba wajumbe waliokuwa wakiandamana na Rais Xi walinunua viwango vikubwa vya pembe hizo.
Uuzaji wa Pembe za ndovu ulipigwa marufuku mwaka 1989 ili kuwazuia wawindaji haramu kuwaua ndovu. (CREDIT: BBC SWAHILI)




Post a Comment