Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Ni mwanamke ndiye aliyelifanya kundi la Wanaume TMK kumeguka!

 


Kundi la Wanaume TMK aka ‘wazee wa mapanga shaaa’ lilijichukulia umaarufu mkubwa enzi likiwa na members wote waliolianzisha.



Hata hivyo kundi hilo lilikuja kuvunjika na kuzaliwa makundi mawili, Wanaume Halisi linaloongozwa na Juma Nature na TMK Wanaume Family ambalo lipo chini ya Said Fela likiwa na wakali kama Chege na Mheshimiwa Temba. Na sasa imebainika kuwa ni mwanamke ndiye aliyewakosanisha jamaa hao.
“Tatizo wote tulivurungwa na ujana mwisho wa siku tukatoa chance kwa watu na wamechukua nafasi,” Amesema Fela.
“Siwezi kusema sio au ndio, lakini huyo mwanamke ameshinda ametushawishi mpaka kubomoa, maana yake ni sawa sawa mwanamke anatumwa kwenda kubomoa nchi. Viongozi kama tunagombania nchi kwaajili ya mwanamke basi tulifeli sisi upande wetu,” alisisitiza.
Jumatatu hii Mheshimiwa Temba amepost picha ya Wanaume TMK kabla halijameguka na kuandika ‘Kabla shetani hajapita.”
Fela amedai kuwa anapanga kuzungumza na Nature ili waendelee kufanya kazi tena.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top