Wasanii wakielezea kifo cha mabovu , Juu ni Msanii Mabovu enzi za uhai wake
Waombolezaji wakiwa na jeneza la msanii Mabovu kutoka msikiti wa Mwangata kwenda makaburi ya Mlolo Iringa
Baadhi ya wasanii wa kundi la Weusi ambao wamefika Iringa kumzika msanii Mabovu leo
Makini akichangisha rambi rambi
Msanii JOh Makini akiwa na michango ya msiba wa mwenzao Mabovu leo
Mwakilishi
wa wasanii wa kundi la Weusi Joh Makini kushoto akimpa pore baba wa
msanii Mabovu mzee Upete kulia baada ya kumaliza kuzika nyumbani kwake
Mwangata wengine ni baadhi ya wasanii walioshiriki mazishi hayo leo
Picha na habari na kikosi cha matukiodaima.co.tz
Vituko
vyatawala msiba wa msanii Ahmed Zubery Upete a. k. a Geez Mabovu Iringa
mlevi (pichani aliyekaa chini)atembeza kichapo kwa wafiwa kisa ataka
aruhusiwe kuufukua mwili wa marehemu ili auage Mara ya mwisho asisitiza
kuwa marehemu amekua nae na ana siri nzito ya kifo chake.
Tukio hilo limetokea muda mfupi baada ya mwili wa marehemu kuwasili makaburi ya Mlolo nje kidogo ya mji wa Iringa kwa mazishi.
Chapombe
huyo ambae alifika makaburini hapo kwa kuchelewa alivamia eneo hilo la
mazishi kwa kuanza kutoa lugha za matusi ya nguoni kwa wafiwa kwa madai
wamewezaje kumzika marehemu huyo bila ya yeye kufika eneo hilo.
Kutokana
na lugha hizo za matusi iliwalazimu Vijana waombolezaji kumtoa kwa nguvu
eneo hilo na kwenda nae pembeni kidogo kumsihi asifanye vurugu kabla ya
chapombe huyo kuanza kurusha Ngumi kwa wasanii.
Akizungumza
mara baada ya mazishi hayo mmoja kati ya wadau wa tasinia ya
muziki nchini na promota mkubwa wa mziki nyanda za juu kusini Edwin
Bashir ambae ni mtangazaji wa kituo cha Radio Ebony Fm alisema
kuwa mbali ya umoja ambao wasanii wameuonyesha katika msiba huo kwa
kuja kushiriki mazishi ila bado angeshauri wasanii kwa wakati
mwingine kujenga ushirikiano wa kumjulia hali mwenzao pindi anapoumwa.
” Sisemi
kwa ubaya ila kiukweli msanii Geez Mabovu ameumwa sana karibu
mwaka mzima anasumbuliwa na ugonjwa wake ila hakuna msanii ambae
amefika kumjulia hali ila leo wengi wamesafiri kuja kumzika…..
inapendeza kusaidiana wakati wa ugonjwa badala ya kusubiri mwenzenu
afe “
Bashir
alisema kuwa msanii huyo ni miongoni mwa wasanii wa mwanzo zaidi
kuutangaza mkoa wa Iriga katika tasnia ya muziki na kuwa hata kabla ya
vituo vya radio kuanzishwa mkoani Iringa alikuwa akiutangaza mkoa na
kusikika katika radio mbali mbali za nje ya Iringa.
Alisema
kuwa msanii huyo toka amemaliza elimu yake kamwe hajapata kufanya
shughuli nyingine nje ya mziki na kuwa wakati wote alikuwa
akijishughulisha na muziki zaidi .
Hata
hivyo alisema chanzo cha Mabovu kuhama mkoa wa Iringa na kuhamishia
makazi yake jijini Dar es Salaam ni kuzidi kuutangaza muziki zaidi
na mkoa wake wa Iringa malengo ambayo alipata kufanikiwa kwa kiasi
kikubwa .
” Utaona
jinsi ambavyo msiba wake leo ulivyowavuta watu wegi wapenzi na
wadau wa muziki kutoka mikoa mbali mbali ya nje ya Iringa ambao
kimsingi baadhi yao imekuwa ni mara yao ya kwanza kufika Iringa
….pamoja na kufarijika kwa umati wa watu waliofika kumzika ila moyo
umeniuma sana hasa ukizingatia kuwa kifo chake hakikuwa na ghafla
bali amekufa kwa mateso makubwa kwa kuugua karibu mwaka mzima sasa
hivyo kwa umoja huo ningetegemea wangefika enzi za uhai wake
kumuuguza mwenzao”
Kwa
upande wake mwakilishi kwa kundi la Weusi Bw Joh Makini alisema
kuwa kifo cha Mabovu kimeacha pengo kubwa katika tasnia ya muziki
hasa muziki wa hiphop Tanzania,
Alisema
kuwa Mabovu amepata kuishinae Kinondoni Jijini Dar es Salaam mtaa
mmoja ila pia amepata kushirikiana kazi mbali mbali za kimzuki .
Hivyo
alisema kuwa ushirikiano huo ndio ambao umewasukuma kufika mkoani
Iringa kushiriki mazishi hayo baada ya pengo kubwa ambalo wamelipata
.
Akizungumza
kwa niaba ya wasanii wazawa na mkoa wa Iringa msanii Squza,alisema
kuwa Iringa imempoteza msanii mkongwe na kuwa kifo chake
kitaenziwa na wasanii wa mkoa wa Iringa pia ambao wapo nje ya mkoa
huo kwa kuangalia jambo la kufanya katika kuwanyanyua wasanii
chipukizi wa mkoa huo.
Alisema
kuwa wapo wasanii maarufu wengi kutoka mkoa wa Iringa ambao wana
majina makubwa kama Rehema Chalamila (RAY C} akina MiKe T na wengine
wengi na kuwa kama njia ya kumuenzi Mabovu watahakikisha
wanaunganisha nguvu kwa kushirikiana na vyombo vya habari kuona
Iringa inampata mwakilishi mwingine wa Mabovu kutoka kwa wasanii
Chipukizi .
Msanii
Mabovu alifariki dunia jana majira ya saa 2 usiku nyumbani kwa
wazazi wake eneo la Mwangata mjini Iringa ambako alikuwa akiugulia na
amezikwa leo katika makaburi ya Mlolo nje kidogo na mji wa Iringa


Post a Comment