Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wema Sepetu Aanika Kisa Cha Kuachana na Diamond

 

MISS Tanzania 2006/07 ambaye ni staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’, amevunja ukimya kwa kuamua kuanika kisa cha yeye kummwaga aliyekuwa mwandani wake, nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Akizungumza na Amani katika mahojiano maalum jijini Dar, juzikati, Wema alianza kwa kufunguka kwamba, kuna watu wamekuwa wakizungumzia ishu ya yeye kumtema Diamond huku kisa wakiwa hawakijui na wengine wamehamishia sababu kwa nyota wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari’, jambo ambalo si kweli.
Wema alimwaga ‘ubuyu’ kwamba, yeye ameamua kumpa likizo ndefu Diamond ili kila mmoja aweze kufanya mambo yake ya maana kwa uhuru mkubwa hasa baada ya jamaa huyo kunukuliwa na magazeti akisema hana mpango wa kuoa jambo ambalo lilimkatisha tamaa na kumwacha njia panda.

Kuhusu suala la kusema amempa likizo ndefu ili kila mtu afanye mambo yake, Wema alirejea safari yake ya China hivi karibuni ambapo Diamond hakutaka asafiri ila akalazimisha. Hapo aliona anatakiwa kuwa huru zaidi.

Wema alipotakiwa kutaja mwisho wa likizo hiyo endapo ni ya siku 28 kama ilivyo kwa sheria ya kazi ya Tanzania, aligoma kusema chochote huku akisisitiza amempa likizo Diamond.

Staa huyo asiyekaukiwa na matukio, alikwenda mbele zaidi kwa kumzungumzia Zari ambapo alisema kuna wanaodai mwanamuziki huyo tajiri yuko kimapenzi na Diamond, lakini yeye haoni ukweli wowote kwani anajua wawili hao wana ‘projekti’ ambayo ni mawazo ya muda mrefu.

“Kwanza naomba watu wajue kuwa, projekti ya Diamond na Zari ninaijua na bahati nzuri Zari ni shoga‘ngu tangu kitambo hivyo yote yanayofanyika mimi nayatambua hatua kwa hatua pamoja na kwamba sijaongea na Diamond siku nyingi,” alisema Wema.

Baada ya mazungumzo na Wema, mwanahabari wetu alimtafuta Diamond kwa lengo la kutaka kumfahamisha kama anafahamu kwamba amepewa likizo ndefu.
“Dah! Nashindwa niseme nini hapo! Lakini ujue maisha kila mfa maji siku zote haishi kutapatapa, kiukweli mimi hapo naona Wema anatoa majibu ya kisiasa tu.
“Nashindwa kujibu kila linalosemwa na watu ila kuna kipindi mtu hutakiwi kujibu kila kitu. Kuna mambo mengine yanatakiwa uyaache yapite tu.

“Mimi nimeachwa na Wema, Zari ni rafiki yangu tu, acheni projekti iendelee,” alisema Diamond huku akichekacheka .

Wakati Diamond akisema hayo, baadaye kwenye maelezo yake mafupi (profile) ya WhatsApp aliweka picha ya Zari huku akiambatanisha na maneno yaliyosomeka:
“Unapokosa usisikitike, Mwenyezi Mungu kakuandalia kizuri zaidi.”
Wema na Diamond wamekuwa na kasumba ya kuachana na kurudiana hivyo kuna kila dalili wawili hao wakarudiana tena.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top