BENDI
inayokuja kasi hapa nchini, Yamoto Band" kundi la vijana wenye vipaji
vipya usiku wa kuamkia leo imefanya kufuru ndani ya Ukumbi wa Burudani
wa "Lina's Night Club" uliopo hapa Mjini Bukoba. Ambao waliimba nyimbo
zao matata za 'Najuta' ya Yamoto Band na nyingine zinazounda Album zao
na kuhudhuriwa na umati wa Mashabiki ndani ya ukumbi huo na kuwafanya
mashabiki muda wote kuvamia jukwaa kwa Makamuzi hayo ya kufa Mtu. Yamoto
Band ambao ndio kwa mara ya kwanza kuja Hapa Mjini Bukoba wakiletwa na
kampuni ya Shemeji Investment kushiriana na Ibra Cadabra.Taswiara ya Mashabiki Waimbaji wa Kundi zim la Yamoto Band wakilishambulia jukwaa!!Mambo ya Yamoto Band...Vijana kazini Bukoba!Mmoja wa Wachezaji wa Bendi hiyo akicheza mbele ya Meza kuu
Wakali
hao ambao walikuwa hawajawahi kupiga shoo yoyote ndani ya Mji wa Bukoba
waliachia radha mpya ambayo ilikuwa haijawahi kupatikana kwenye Kiwanja
hicho cha Maraha Lina's Night Bukoba.
Vijana
hao wa kundi la Yamoto bendi lenye masikani yake TMK jijini Dar es
salaam wanaotishia bendi kongwe za hapa nchini, Yamoto Band chini ya
Prezidaa wake, Dodo Aslay walivamia jukwaa na kudhihirisha kuwa wamekuja
kuushika muziki wa dansi hapa nchini na kuwaambia Wakazi wa Bukoba
waliopata nafasi ya kuwaona live kuwa Wamakuja kufanya kazi ya kutoa
Burudani yakutosha.
Baadhi ya Mashabiki waliohudhuria kwa makini wakiwaangalia Vijana JukwaaniMashabiki wakiwanyanyulia Mikono juu Wasamii waKundi hilo la Yamoto Band kwenye Ukumbi wa Lina's usiku wa kuamkia leo.
Vijana hao waliwapagawisha mashabiki kwa nyimbo zao mbalimbali kama vile Yamoto, Birthday na nyingine kibao.
Mmoja
wa Waandaaji wa Show hii kutoka kampuni y Shemeji Investment Mr. Jerry
Maarufu kwa jina la Mc akishangaa jukwaani Vijana wanavyokamua na
Mashabiki walivyounga mkono kuingia kwa Wingi katika Ukumbi huo wa
Lina's Club Bukoba mjini.
Mashabiki walikosa viti na wengine kuvisimamia baada ya kufunikwa nyomi la Watu waliokuwa mbele yao.
Wengine walisimama kwenye kuta ili waweze kuona vizuri mbele
Wakina dada wakichukua picha kwenye simu zao
Mzungu wa Bukoba nae hakuweza kujificha
Post a Comment