MWANAMUZIKI wa muziki wa Bongo Fleva
nchini, Nasib Abdul, Diamond Platinum
anashindana na aliekuwa mpenzi wake Wema Sepetu katika kuwania Tuzo ya
Mtu mwenye ushawishi mkubwa katika mitindo.
Tuzo hiyo zitatolewa kwenye Onesho la
Mavazi la Swahili Fashion 2014 linaloandaliwa na Kampuni ya 361 Degrees na zitatolewa
siku ya mwisho katika onesho la Swahili Fashion Week litakaloanza Desemba 5
hadi 7 mwaka huu.
Katika shindano hilo wanaoshindana
wengine ni pamoja na Mwamvita Makamba ambae
namba yake ya kupigiwa kura ni SFW SY 01, Diamond Platnumz SFW SY 02, Millen Magesse SFW SY 03, Mohamed Dewji SFW SY 04 na Wema Sepetu SFW SY 05.
Pia Diamond anashindana katika
kipengele cha wanaume wenye kuongoza huku namba yake ya ushiriki ikiwa ni SFW
SMP 01 na anaochuana nao katika kipengele hicho ni pamoja na Luca Neghesti SFW SMP 01, Baraka Shelukindo SFW SMP 03, Noel Ndale SFW
SMP, Rio Paul SFW SMP 05 na Juma Juxx SFW SMP 06
Akizungumza na waandishi wa habari
mratibu wa tuzo hizo, Haruna Ibrahim alisema kuwa kwa mwaka huu kuna ushindani
mkubwa katika kila kipengele. Aliongeza kuwa Meneja wa Msanii Wema
Sepetu, Martin Kadinda nae anawania kipengele cha Mbunifu bora wa mchango
katika tasnia hiyo ambapo anashindana na
akina PSJ Couture SFW MWD 01.
Martin Kadinda. SFW MWD 02 Mtani Nyamakababi SFW MWD 03, Manju Msitta SFW MD 04 na Gabriel Mollel SFW MWD 05.
Aliongeza kuwa pia kwenye kipengele
cha mbunifu wa mavazi bora wa mwaka wanaoshindania Kadinda anashindana akiwa
anaumana na akina Gabriel Mollel SFW
ID 02, An Nisa Abayas SFW ID 03, Eve
Collections SFW ID 04
Alisema kuwa kwa upande wa Baileys,
mwanamitindo bora wa kike kwa mwaka huu wanaoshindana ni Jamilla Nyangassa ambae namba yake ya kupigiwa kura ni SFW
FM 01, Gyver Meena SFW FM
02, Jihan Dimachk SFW FM 03, Neema Kilango SFW
FM 04, Joceline Maro, SFW FM 05,
Lethina Christopher SFW FM 06.
Kwa upande wa wanamitindo bora wa
kiume wanaoshindania tuzo hizo ni pamoja na Danny David SFW
MM 01, Victor Casmir SFW MM 02, Dietrich
luhanga SFW MM 03, Ally Daxx SFW
MM 04.
Haruna aliongeza kuwa kwa upande wa
Tuzo za Mwanamitido bora wa mwaka kwa Afrika Mashariki wanaoshindaniwa ni
pamoja na Vivian Mutesi (UGANDA) SFW
EAM, Sharon Mirembe Sanya (UGANDA) SFW
EAM 02, Christina Masese (KENYA) SFW EAM
03, Ajuma Nasenyana (KENYA) SFW EAM
04
Aliongeza
kuwa kwa upande wa Tuzo ya Mbunifu wa mwaka wanaoshindania ni pamoja na Kiki's
Fashion SFW DY 01, Jamilla Vera Swai SFW DY 02, Ailinda Sawe SFW DY 03,An Nisa Abayas SFW DY 04, Manju Msita SFW DY 05, Lucky Creations SFW
DY 06
Pia aliongeza kuwa kutakuwa na tuzo
ya mwaka kwa mtaalamu wa urembo na nywele na wanaoshindaniwa ni pamoja na Rehema
Samo SFW HMA 01, Asila Makeup SFW HMA 02, Glambox SFW HMA 03, Lavie Makeup Studio SFW HMA 04.
Pia wanaoshiriki katika kipengele cha
kushindani tuzo ya vidani ni The Mabinti Center
SFW AD 01, Enjipai Jewelleries SFW AD 02, Florinyah Designs SFW AD 03, Sairiamu SFW AD 04, Linda August SFW AD 05 na Nyumbani Designs SFW
AD 06.
Watakaoshindania tuzo katika
kipengele cha mbunifu wa Afrika Mashariki wanaoshindania ni pamoja na Martha Jabo (Uganda) SFW EAD 0, Afrostreet Kollektions
(Kenya) SFW EAD 02, Arapapa by Santa
Anzo (Uganda) SFW EAD 03,
Akinyi Odongo (Kenya) SFW EAD, Kiko Romeo
(Kenya) SFW EAD 05 na Mille
Colliness (Rwanda) SFW EAD 06.
Swahili
Fashion Week na Tuzo za mwaka 2014 zinaandaliwa na 361 Degrees kwa usaidizi wa Hotel
Sea Cliff, Sea Cliff Court, chini ya udhamini wa EATV, East Africa Radio,
Baileys, Mercedes-Benz, 2M Media,
Tanzania Printers LTD and Syscorp Media na Basata.
Post a Comment