Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Idadi ya waliopoteza maisha kufuatia mafuriko wilayani Kahama yaongezeka na kufikia 46.


Idadi ya watu waliopoteza maisha katika mafuriko ya mvua ya mawe iliyonyesha katika kata ya mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeongezeka na kufikia watu 46 huku idadi ya majeruhii waliopelekwa hospitali ikipungua baada ya kutibiwa na kuruhusiwa kuondoka.
Hayo yamebainishwa na mbunge wa jimbo la msalala Ezekiah maige wakati akizungumza katika mahojiano maaalum kabla ya kumpokea waziri mkuu ambapo amesema kati ya majeruhi 91 wanne wamepoteza maisha na kufikia idadi ya vifo hadi sasa kuwa 46.
 
Akitoa taarifa ya serikali waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera uratibu na bunge Mh. Jenista Mhagama amesema serikali ipo tayari kuhudumia waathirika kwa misaada mbalimbali ikiwemo chakula na vifaa muhimu na kuwataka kamati ya maafa mkoa ihamishie ofisi za uratibu katika eneo la tukio ili waathirika wapate huduma kwa wakati.
 
Akitoa rambirambi za serikali waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda amesema serikali imekuja na timu ya waratibu watakaoratibu mahitaji kwa waathirika ili waweze kusaidiwa kwa kutumia ghala la chakula la kanda lililoko shinyanga kutoa chakula na hakuna atakayekosa chakula.
 
Baadhi ya waathrika wameeleza pigo walilopata kwa kuondokewa na ndugu katika familia zao pamoja na kuachwa bila  hata makazi ya kuishi achilia mbali mashamba kufagiliwa na mvua hiyo hatari ya upepo na mawe.
 
chanzo:itv
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top