Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SERIKALI YACHUKUA HATUA KUKABILIANA NA MAAFA KAHAMA


Kufuatia mvua kubwa zilizonyesha usiku wa tarehe 04 Machi, 2015 Wilayani Kahama mafuriko makubwa yalitokea na kuathiri wakazi wa kata ya Mwakata katika vijiji vya Mwakata, Numbi na Mwaguguma. Kutokana na mafuriko yaliyotokea tathmini ya awali inaonesha kuwa watu 42 wamepoteza maisha, watu 82 wamejeruhiwa na watu wanaokadiriwa kufikia 574 wameathirika. Jumla ya nyumba 137 zimeathirika kwa viwango mbalimbali.

Serikali imechukua hatua za haraka kwa kushirikiana na wananchi kuwafikia na kuwanusuru waathirika wa mafuriko hayo waliokuwa wamezingirwa na mafuriko. Aidha vimeanzishwa vituo vya muda kuwahifadhi wananchi hao kwenye Shule.
Serikali imepeleka misaada ya kibinadamu kama ifuatavyo;
i. Chakula tani 20. Maharage tani 5, Mafuta ya kupikia lita 1,126 na Sukari tani 1.3
ii. Vifaa vya matumizi ya ndani ambayo vinajumuisha blanketi 650, ndoo 82 za lita 20, ndoo 82 za lita 10 ; Vifaa vya kupikia seti 82 na madumu 82
Kwa kuwa bado Serikali inalo jukumu kubwa la kuwawezesha waathirika kurejea katika maisha yao ya kawaida; inapenda kuwatangazia wale wote wanaoguswa na maafa haya kuwa Serikali inaendelea kupokea misaada mbalimbali ambayo inahitajika kwa waathirika.
Mahitaji haya ni pamoja na sare za shule; daftari za wanafunzi; mavazi ya kike na kiume; na chakula. Aidha kwa kuzingatia kuwa waathirika hawa wamepoteza mali na fedha katika maafa haya; misaada ya vifaa vya ujenzi (sementi, mabati, mbao, n.k.) inahitajika sana.
Utaratibu wa kupokea misaada hiyo kwa walio Dar es Salaam wanaweza kuiwasilisha misaada hiyo Idara ya Kuratibu Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu au kuwasiliana na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga_ Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Serikali itaendelea kuwasaidia Waathirika dhidi ya Changamoto zinazoweza kujitokeza hususani za kiafya zinazosababishwa na uchafuzi wa vyanzo vya maji na mazingira. Elimu juu ya ujenzi wa nyumba bora na makazi maeneo salama itaendelea kutolewa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top