Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Majambazi Yavamia Kanisani na Kuiba Chombo Kinachotumika Kuhifadhia Ekaristi Takatifu......Kwa Mujibu wa Sheria Za Roma, Ukristo Ndo Basi Tena Eneo Hilo



Watu watano wamevamia na kuvunja madirisha ya Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Malolo na kuiba chombo kinachotumika kuhifadhia ekaristi takatifu (TABERNACULO).
 
Imeelezwa kuwa majambazi hayo yalidhani chombo hicho kimetengenezwa kwa dhahabu.
 
Tukio hilo lilitokea juzi, saa 8:30 usiku, baada ya majambazi hayo kuvunja madirisha ya kanisa hilo.
 
Kanisa hilo ni miongoni mwa makanisa makongwe na yenye historia kubwa hapa nchini, ambalo lilijengwa mwaka 1939.
 
Paroko wa kanisa hilo, Theophan Membe, alisema siku ya tukio alikuwa Lindi kuhudhuria misa takatifu ya mapadre wa jimbo la Lindi, iliyoongozwa na Askofu wa jimbo hilo Mhashamu Bruno Ngonyani.
 
Alisema baada ya tukio hilo alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kigango cha Malolo, Cleophas Nnonjela, na badaye walitoa taarifa polisi.
 
Membe alisema parokia ya Malolo ni miongoni mwa parokia zilizotoa wasomi wengi mkoani Lindi kutokana na historia yake.
 
Alisema kwa mujibu wa sheria za Roma za kanisa hilo, sehemu inayoibiwa Tarbenaculo, ukristo hufa mpaka wahusika walioiba kifaa hicho watakapokiri kuwa wameiba.
 
Membe alisema baada ya wahusika kukiri kama wameiba, askofu wa jimbo anaondoa dhambi ya mauti kutoka kwa waumini kwenda kwa wezi hao.
 
Alisema kutokana na kuibiwa kifaa hicho, waumini wa kigango hicho watakosa baadhi ya huduma ikiwemo ibada ya Jumapili, misa ya kila siku asubuhi, misa ya katekista na upigwaji wa kengele zinazoashiria saa kwa waumini.
 
Alisema katika kipindi hicho huduma za ubatizo, kipaimara, komunio takatifu, kitubio, misa za mazishi, mpako kwa wagonjwa, sherehe za ndoa na masuala yote ya msingi yanayohusu Kanisa Katoliki hayatakuwepo.

 PAROKO wa kanisa katoliki parokia ya Malolo padre THEOPHANI MEMBE ambaye ameonesha kukerwa na kitendo kilichofanywa na Watu hao ambao mpaka sasa hawajulikani huku akiahidi kusitisha huduma ya ibada kwenye kigango hicho.
 KANISA Takatifu la Mtakatifu JOSEPH MFANYAKAZI Parokia ya Malolo Jimbo la Lindi katika mkoa wa Lindi ambamo TARBENACULO hilo limeibiwa na watu wasiofahamika.

 NYUMBA anayoishi Paroko wa parokia ya Malolo Fr.Theophan Membe ambayo Mlango wake kwa huko nyuma umevunjwa na watu wasiofahamika waliokuwa na lengo la kuiba.
 ASKOFU wa Jimbo la Lindi Mhashamu BRUNO NGONYANI ambaye anasubiriwa kutangaza adhabu kwa waumini wa kanisa katoliki kigango cha Malolo wakati wowote kutoka sasa mpaka pale waliohusika watakapokiri mbele ya waumini.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top