CH10 NEWS
Umoja
wa Vyama vya umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, wamshauri raisi Kikwete
kuto saini miswada ya mafuta na gesi kwa maslahi ya taifa. http://youtu.be/b0cf6mJxYJA
Waziri
wa mambo ya ndani Mathias Chikawe, asema usalama wa nchi ndani na
mipaka ni madhubuti na wananchi waendelee na ujenzi wa taifa. http://youtu.be/1NhCGk7W5nc
Kiwango
cha maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi kimeshuka kwa kiasi kikubwa
kufuatia juhudi za serikali na baadhi ya taasisi katika kutoa elimu
dhidi ya ugonjwa huo. http://youtu.be/NdwvPa9tvjk
Tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC, yataja majimbo mapya ya uchaguzi na kubadili mipaka iliyokuwepo awali. http://youtu.be/rs9-FmUO5Zg
Serikali
yapiga marufuku makundi ya wapambe wa wagombea yaliyoandaliwa kuelekea
Dodoma kushuhudia uteuzi wa wagombea wao huku hatua kali zikitolewa
dhidi yao. http://youtu.be/Eu8gqh4Ex28
TBC NEWS
Spika
wa Bunge Anne Makinda aishauri serikali kujenga mfumo imara wa nidhamu
katika usimamizi na matumizi ya fedha za gesi nchini. http://youtu.be/M5HzjhxvEIc
Jeshi
la polisi mkoani Tabora laendesha operesheni maalum kukamata watu
waliovamia msitu wa igombe na kufanya uharibifu mkubwa na kuhatarisha
Bwawa la Igombe. http://youtu.be/-WWqSJRFqTI
Viongozi
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wausogeza mbele uchaguzi wa wabunge na
uraisi ili kuweza kupata muda wa kuujadili uchaguzi huo. http://youtu.be/5nW8okoqIQ8
Makamo
wa pili wa Raisi Dr.Bilal asema utumiaji wa mbegu bora nchini na Afrika
kwa ujumla si mzuri kutokana na kutumia kiwango kidogo cha mbegu zilizo
zalishwa katika vituo vya utafiti. http://youtu.be/0BaV8jjwhE4
Jaji mkuu wa Tanzania Othman Chande asema idara ya mahakama inazidi kuboresha huduma zake ilikuwa karibu zaidi na wananchi. https://youtu.be/PZKbXlABi1U
STAR TV NEWS
Kufuatia adhabu iliyotolewa kwa wabunge wa upinzani, wabunge wote wa UKAWA waadhimia kutohudhuria vikao vyote vilivyobakia. http://youtu.be/cMNq8IW44vk
Jeshi
la polisi Mkoani Morogoro linawashikilia watu 2 kwa kukutwa na silaha
aina ya shot-gun wakiwa katika maandalizi ya kufanya uhalifu. http://youtu.be/O0eIBivlMQM
Wakati
siku za kuelekea uchaguzi mkuu zikiyoyoma, mgombea uraisi na mhadhiri
Mchungaji Malisa abadili azimio lake la awali na kuhaidi kugombea
kupitia chama cha CCK. http://youtu.be/a0IKvinUQ1U
Wizara
ya mambo ya ndani imefanikiwa kuwafuta kazi askari polisi 70 na askari
uhamiaji 21 baada ya kubainika kujihusisha na vitendo vya rushwa katika
awamu ya 4. http://youtu.be/VJDdJZd2xLA
AZAM TV NEWS
Raisi Nkurunzinza wa Burundi asusia kikao maalum cha wakuu wa EAC jijini Dar es salaam huku akiwakilishwa na waziri wake.http://youtu.be/jabCkjKdFXg
Wakulima wa zao la korosho hapa chini waeleza kukumbwa na changamoto kubwa inayowafanya washindwe kushindana kimataifa. http://youtu.be/jK8gglVO4Uo
Jamii
ya watu wenye ulemavu yashauriwa kuachana na fikra za utegemezi
kutokana na hali walizo nazo jambo ambalo linawafanya wajikute wakiwa
ombaomba. http://youtu.be/GtXRPXxz9K8
Msanii wa nyombo za Taarabu, Mzee Yusuph atangaza nia ya kuwania ubunge huko Zanzibar. http://youtu.be/4Eh442-J89E
Zoezi
la uandikishaji BVR visiwani Zanzibar limekalima mwishoni mwa wiki huku
vyama vikuu vya upinzani vikilalamikia jinsi zoezi hilo lilivyo
endeshwa. http://youtu.be/onTj6UuK_Vw
Post a Comment