Aliyeshindwa
ujumbe wa NEC Ludewa Injinia Zephania Chaula akiangana na mbunge Deo
Filikunjombe baada ya kushindwa katika nafasi hiyo ,Chaula alikuwa ni
mmoja wa wana CCM waliokuwa wakitaka kuwania ubunge jimbo la Ludewa
Chaula akiagana na mshindi mzee Nkwera
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Antonia Choya akimkabidhi hati ya shukrani mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe (kushoto)
Mjumbe wa mkutano huo Bw Choya akipiga kura.
Wajumbe wakishiriki kupiga kura.
Wajumbe wakishiriki kupiga kura
Mgombe Chaula akishukuru kwa kushindwa
Injinia Chaula akimpongeza mshindi mzee Nkwera.
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akipiga kura kumchangua mjumbe wa NEC Ludewa
MBIO za ubunge jimbo la Ludewa mkoani Njombe zimeishia hewani kwa mtangaza nia wa wanafasi hiyo Injinia Zephania Chaula baada ya kuambilia kura 11 pekee katika nafasi ya mjumbe wa Halmashauri kuu ( NEC) Taifa kutoka wilaya ya Ludewa aliyokuwa akiwania dhidi ya katibu msaidizi wa mbunge wa jimbo la Ludewa Hilaly Nkwera aliyeibuka mshindi kwa kupata kura 138 kati ya kura zote halali 151 zilizopigwa .
Huku
mgombea huyo aliyeshindwa katika nafasi hiyo ya Ujumbe wa NEC Injinia
Chaula akiapa kutogombea tena nafasi hiyo kwa madai kuwa ni mara ya
pili sasa anashindwa vibaya katika mchakato
wa kuwania nafasi hiyo ambapo awali alishindwa mgombea wa darasa la saba marehemu Elizabeth Haule .
Uchaguzi huo
mdogo wa kuziba nafasi ya mjumbe wa NEC iliyoachwa wazi
na aliyekuwa mjumbe wa nafasi hiyo Elizabeth Haule aliyefariki
dunia mapema mwaka huu ,ulifanyika mwishoni mwa wiki hii
kwa kuwashirikisha wagombea hao wawili kabla ya mgombea mwingine
ambae ni mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kuandika barua
ya kujitoa katika kinyang’anyiro hicho akiwapisha wagombea
hao wachuane kutokana na yeye kudai kuwa atachukua fomu ya kugombea
tena ubunge wa jimbo hilo la Ludewa .
Akitangaza matokeo
hayo ya uchaguzi msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Lucas Nyanda ambae
ni katibu wa jumuiya ya wazizi wa CCM mkoa wa Njombe ,alisema
kuwa jumla ya wajumbe waliopaswa kushiriki katika uchaguzi huo ni
164 ila wajumbe halali walioshiriki ni 151 na kati ya wajumbe hao
kura 2 ziliharibika huku Injinia Chaula akipata kura 11 na mshindi wa
nafasi hiyo Bw Nkwera akipata kura 138
Awali mbunge wa jimbo la Ludewa Bw Filikunjombe ambae alikuwa ni mmoja kati ya wana CCM watatu ambao majina yao yalirejeshwa kuwania nafasai hiyo alisema kuwa analazimika kujitoa katika nafasi hiyo ili kupisha wanachama hao wawili ambao wamemzidi umri ili kuweza kupambana na yeye ataendelea kuwa kuwatumikia wananchi wa Ludewa katika nafasi ya ubunge pekee.
Akiwashukuru
wajumbe kwa ushindi huo wa nafasi ya ujumbe wa NEC Bw Nkwera
ambae kitaaluma ni mwalimu na pia amepata kuwa mwenyekiti wa
Halmashauri ya wilaya ya Ludewa na mwenyekiti wa madiwani wa mkoa wa
Njombe na Iringa alisema kuwa amefurahishwa na imani kubwa ambayo wana
CCM wameionyesha kwake kwa kumchagua kuwa mwakilishi wao katika
vikao vya kitaifa .
Bw Nkwera alisema wana CCM Ludewa waamini kuwa nafasi hiyo hawajakosea kumpa na kamwe hatawaangusha kwani atahakikisha anawatumikia vema katika vikao vya juu kwa kuanza na safari ya kumpata mgombea wa nafasi ya Urais wa CCM ambae atakuwa ni chaguo la wana CCM wote wa Ludewa .
Post a Comment