Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MTANZANIA ALIYEPATA TUZO YA MALKIA ELIZABETH II ATOA TAMKO


Mshindi wa tuzo za The Queens Young Leaders, mwanamke kutoka Mkoa wa Mwanza, Angela Benedicto ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Kwotesawa linalohusika na kutetea haki za watoto (kushoto) Mshindi wa tuzo hizo (anayezungumza), Given Edward pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma za Teknolojia, Eng. Peter Phillip.
Wanahabari wakichukua tukio. ...Angela akitoa…
Mshindi wa tuzo za The Queens Young Leaders, mwanamke kutoka Mkoa wa Mwanza, Angela Benedicto ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Kwotesawa linalohusika na kutetea haki za watoto (kushoto) Mshindi wa tuzo hizo (anayezungumza), Given Edward pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma za Teknolojia, Eng. Peter Phillip.Wanahabari wakichukua tukio. ...Angela akitoa ufafanuzi.
MTANZANIA aliyepata tuzo ya Malkia Elizabeth II, Given Edward  ambaye alitwaa tuzo hiyo leo ametoa tamko juu ya tuzo aliyoipata kutokana na kutengeneza Mtandao wa kujadiliana  wanafunzi kimasomo  kupitia mtandao huo.
Akizungumza na wanahabari jana katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) Given  Edward amesema yeye ni miongoni wa watanzania 9 waliokuwa wamechaguliwa na nchi za jumuiya ya  madola ambazo zilitangaza kutengeneza ‘project’ mitandao ya kijamii ambapo aliibuka kidedea.
Alisema kuwa katika vijana hao 9 wa kitanzania aliweza kuibuka kuwa mshindi wa kwanza wa tuzo hizo zijulikanazo kama ’The Queenns Young Leaders’ ambapo alitengeneza project ya mtanadao ujulikanao kama ‘My Elimu’ ambao lengo lake ni kuwakutanisha wanafunzi pamoja kutoka nchi mbalimbali kuweza kusoma kwa kutumia mtandao huo pasipo kuwa sehemu moja.
“Mtandao huo ni nafuu sana kwa kizazi cha sasa kwani unamrahisishia mwanafunzi kuweza kujadiliana masuala mbaliambali ya kielimu, namana ya kukokotoa maswali bila kusafiri kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine pasipo bila kupoteza mda hivyo nawaombeni watu waufatilie”alisema.
Aliongeza kuwa kadiri siku zinavyokwenda anatarajia kubalidilisha mfumo wa maandishi  kuwa katika picha ili kumwezesha mwanafunzi kuwa katika mfumo wa kileo wa teknolojia na hata kumwezesha aliyepo kijijini kuweza kupata maswali mbalimbali ya masomo papo hapo kwa kutumia mfumo huo wa My Elimu ambao ni wa haraka sana, hivyo akawataka vijana kutembelea mtandao huo wa www.MyElimu kuweza kujifunza zaidi.
HABARI, PICHA: NA DENIS MTIMA/GPL
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top