Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Polisi Yanasa Mtambo Wa Kutengeneza Bunduki



POLISI mkoani Rukwa imewakamata watuhumiwa 19 na silaha za aina mbalimbali zikiwemo bunduki 30, risasi 231 pamoja na mtambo wa kutengeneza bunduki za kienyeji.
 
Katika msako uliofanywa na Polisi mkoani hapa, pia waliweza kukamata nyara za Serikali yakiwemo meno, mikia miwili ya tembo na maganda mawili ya risasi.
 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema jana mjini hapa kuwa silaha hizo zilikamatwa kutokana na operesheni ya kupambana na visa vya ujangili na uhalifu mwingine katika maeneo mbalimbali ndani ya mkoa huu.
 
Alibainisha kuwa silaha hizo zilizokamatwa zinasadikiwa kutumika katika visa vya kijangili na uhalifu mwingine ambapo baadhi ya bunduki zimegundulika kuwa zinamilikiwa kihalali.
 
Alizitaja silaha zilizokamatwa kuwa ni bunduki aina ya shotgun 8, rifle 8, magobori 4, bunduki 6 aina ya shotgun zilizotengenezwa kienyeji, risasi 5 za SMG, risasi 53 za rifle na risasi 173 za shotgun.
 
Kwa mujibu wa Kamanda Mwaruanda watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote baada ya uchunguzi wa awali wa kukamilika.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top