Wakati uvumi wa kujiuzulu cheo na kujivua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, ukiwa umetawala kupitia mitandao ya kijamii na magazeti, taarifa zinadai kuwa sababu ya kuchukua hatua hiyo ni shinikizo kutoka kwa mkewe.
Taarifa
zilizochapishwa na gazeti moja likimnukuu Dk. Slaa mwenyewe, zilisema
ameachana na siasa na kujivua wadhifa wake na atabaki kufanya shughuli
zingine.
Dk. Slaa amedaiwa hakubaliani na namna chama chake kilivyompokea Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa.
Lowassa
aliyekuwa Mbunge wa Monduli alitangaza kuhamia Chadema, Julai 28, mwaka
huu baada ya kutoridhishwa na mchakato wa CCM wa kumpata mgombea wa
urais.
Habari
za uhakika kutoka vyanzo vyetu vya habari ndani ya Chadema zinadai, Dk.
Slaa alishiriki katika mchakato mzima wa kumpokea na kuridhia Lowassa,
kusimamishwa kuwa mgombea urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa).
Hata
hivyo, chanzo kingine cha habari kinadai kuwa mke wa Dk. Slaa,
Josephine Mashumbusi, alitoa shinikizo kwa mumewe la kujiuzulu baada ya
kuruhusu kusimamishwa mgombea mwingine (Lowassa).
"Josephine
alikuwa na uhakika mume wake ndiye atakayesimama ugombea urais kwa
upande wa Ukawa, hali ilivyobadilika, akakasirika na kumwambia mumewe
ama yeye au Chadema," chanzo kilidokeza.
Kupitia ujumbe uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii, unaoonyesha kutoka kwa Mashumbusi, aliandika
"Ni kweli Frida na kwa hili Dk. Slaa amejivua wadhifa wake wa ukatibu
mkuu na kuachana na siasa. Hamtamsikia tena kwani hawezi kupinga
anachokiamini".
Hata
hivyo, Dk. Slaa alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi kuthibitisha
madai hayo, iliita mara moja na kuzimwa. Juhudi za kumpata ziligonga
mwamba baada ya simu yake kutopatikana hali kadhalika simu ya
Mashumbusi.
Wakizungumza
na mtandao huu, baadhi ya wasomi walisema kama Dk. Slaa amejiuzulu
nafasi yake na kujivua unachama atakuwa amejijengea heshima na uaminifu
na kwamba Chadema kitapata pigo.
Mhadhiri
wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, alisema kwa upande
wake aliamini kitu kama hicho kitatokea kutokana na tukio hilo kuwa la
haraka na kulifananisha sawa na mapinduzi ya ghafla ndani ya chama.
“Nafikiri
kama kweli Dk. Slaa amejivua uanachama itakuwa ni jambo zito na pigo
kwa Chadema, lakini ni uamuzi wa busara na kumjengea heshima kwa jamii,” alisema Dk. Bana.
Alisema kitendo cha Lowassa kuhamia chama hicho kwa haraka kilileta mashaka na mijadala kwa baadhi ya viongozi.
“Ninavyojua
mimi ndani ya Chadema kuna watu wenye misimamo na wapo tayari kuilinda
kwa nguvu zote, kujitoa kwake sawa na kutaka kusimamia kile
anachokiamini na kukaa kwake kimya katika jambo hili lazima kutakuwa na
mshindo mkuu,” alisisitiza.
Mhadhiri
huyo alisema anaamini Slaa aliweza kukifufua chama hicho mwaka 2010 kwa
kuweka misingi yake ya kukemea ufisadi, hivyo hawezi kurudi nyuma kwa
kuivunja.
Dk.
Kitlya Mkumbo kwa upande wake alisema anaheshimu maamuzi ya pande zote
mbili kwani zinaonyesha demokrasia na ukomavu wa kisisa.
Alisema
Dk. Slaa amechukua uamuzi sahihi wa kujiuzulu kwa sababu ni haki yake
kikatiba na Chadema wamechukua hatua ya kumkaribisha Lowassa walikuwa na
njia njema kukuza upinzani na kuiondoa CCM madarakani.
Kauli za Slaa Dhidi ya Lowassa
Septemba
15 mwaka 2007 katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam, Dk.
Slaa alimtaja Lowassa kuwa miongoni mwa mafisadi 11 waliochota fedha
Benki kuu katika akaunti ya Epa.
Kauli
hiyo alikuwa akiitamka kila mahali alipokwenda na kusisitiza kwamba
Lowassa na viongozi wenzake wa CCM wamechafuka kwa ufisadi.
Akiwa
katika kampeni ya urais mwaka 2010, Wilayani Monduli Dk. Slaa
alimshambulia Lowassa, kwa kushindwa kudhibiti vitendo vya kifisadi
vilivyotokea jimboni na serikalini.
Akizungumza
katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya Bomani, alisema binafsi
hana ugomvi na Lowassa kwani ni mmoja wa viongozi aliofanya nao kazi
kwa karibu na ni rafiki yake, lakini wanatofautiana katika masuala ya
msingi yanayohusu maslahi ya Taifa.
Post a Comment