Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

DKT. MAGUFULI AZIDI KUNOGESHA KAMPENI ZA CCM ZA URAIS MKOANI RUVUMA‏

                   

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akipanda kwenye tingatinga ishara ya kuonesha uchapakazi wake serikalini.
....Akiliwasha tingatinga. 


Magufuli akiendesha tingatinga linalofanya kazi kwenye barabara inayojengwa kutoka Kijiji cha Kirimasera hadi Matemanga, mkoani Ruvuma.


Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mikono wananchi ikiwa ni ishara ya kuwasalimia alipowasili kwenye mkutano wa kampeni mjini Mbinga, Mkoa wa Ruvuma jana, ambapo aliahidi kuboresha kiwanda cha kukoboa kahawa na kujenga barabara ya lami kutoka Mbinga hadi Mbamba bay.
Magufuli akihutubia wakazi wa Songea mjini kwenye uwanja wa majimaji ambapo aliwaeleza wananchi hao kuwa Serikali yake itafanyakazi kwa ajili ya maendeleo ya watanzania.

 Mbunge wa zamani wa Jimbo la Songea Mjini, Dkt. Emmanuel Nchimbi  akiwaomba wananchi wa Ruvuma kumpigia kura Mgombea urais wa Tanzania kupitiaa CCM, Dkt. John Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni wa CCM kwenye Uwanja wa Maji Maji, mjiniSongea, mkoani Ruvuma.

Magufuli akiwa na watoto aliowapatia zawadi alipokuwa akiondoka baada ya kujinadi katika Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma.

 Mwananchi akimpigia makofi Dkt. Magufuli baada ua kufurahishwa na hotuba yake katika Kijiji cha Kigonsera, wilayani Mbinga, Ruvuma jana.

 Dkt. Magufuli akisalimiana na dada wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Nyasa kupitia CCM, na mhamasishaji Mkuu wa CCM, marehemu Kapteni John Komba, alipokwenda kutoa shada la maua kwenye kaburi  Kapteni Komba katika Kijiji cha Lituhi, wilayani Nyasa, mkoani Ruvuma akiwa katika ziara ya kampeni za urais, ubunge na udiwani

 Dkt. Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Kapteni Komba.

Magufuli na viongozi wengine wa CCM, wakiomba dua kwenye kaburi la marehemu  Kapteni Komba.
 Ngoma ikitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni za urais, ubunge na udiwani katika Kijiji cha Lituhi, Wilaya ya Nyasa.

 Dkt. Magufuli akinadi kwa wananchi katika Mji wa Lituhi, Wilaya ya Nyasa, Ruvuma.

 Dkt. Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Nyasa, Stelah Manyanya katika mkutano wa kampeni katika Mji wa Lituhi.
 Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dkt. Magufuli.
 Dkt. Magufuli akimvisha kofia ya CCM, aliyekuwa Mwenyekiti Mtedaji wa Kijiji cha Kwanza Kata ya Lituhi, kupitia Chadema, Sixbert Nyembo baada ya kutangaza kuwa yeye na wenzie zaidi ya 270 kukihama chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Lituhi, wilayani Nyasa leo

 Wananchi wakimshangilia Dkt. Magufuli katika wakati msafara wake ulipozuiwa katika Kijiji cha Rwanda, wilayani Mbinga.

 Wananchi wakishangilia katika Kijiji cha Amani  walipomuona Magufuli wakati msafara wake ulipozuiwa katika Kijiji hicho kilichopo wilayani Mbinga.

 Msafara wa Dkt. Magufuli ukipita kwenye Barabara mpya ya lami inayotoka Songea kwenda Mbinga.

 Dkt. Magufuli akishangiliwa alipokuwa akiwahutubia wakati wa Kijiji cha Kigonsera waliomzuia alipokuwa akienda kwenye kampeni mjini Mbinga.
 Dkt. Magufuli akiwasamia wananchi alipowasili kwenye mkutano wa kampeni mjini Mbinga.

 Dkt. Magufuli akihutubia wananchi na kutoa ahadi mbalimbali atakazozitekeleza akiwa chaguliwa kuwa rais ambapo alisema kuwa kila kijiji kuanzia mwakani kitapewa sh. mil. 50 za kuwakopesha vijana na akina mama.
 Dkt. Magufuli akimkabidhi Mgombea Ubunge Jimbo la Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda Ilani ya Uchaguzi ya CCM wakati wa mkutano huo wa kampeni.
 Magufuli akionesha Ilani ya Uchaguzi ya CCM kabla ya kumkabidhi mgombea ubunge Jimbo la Mbinga Vijijini wakati wa mkutano huo.

Magufuli akimsalimia mmoja wa walemavu waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni mjini Mbinga

 Sehemu ya wananchi walioshiriki kwenye mkutano wa kampeni za CCM katika Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma jana.

Magufuli akijinadi kwa wananchi wakati wa mkutano wa kampeni katika Jimbo la Peramiho

 Mama mfuasi wa CCM akifurahi baada ya kumsikia Magufuli akiahidi kuanzisha pensheni kwa wazee kuanzia mwakani.

 Mgombea Ubunge Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama akipokea Ilani ya Uchaguzi ya CCM kutoka kwa Mgombea Urais kupitia chama hicho, Dkt. Magufuli wakati wa mkutano huo wa kampeni.

 Magufuli akiwapungia mkono wananchi kuwaaga baada ya kujinadi katika Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma.

 Magufuli akiwapungia mkono wananchi kuwaaga baada ya kujinadi katika Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma



 Sehemu ya wanchi wa Ruvuma wakinyoosha mikono kukubali kumpigia kura Mgombea urais kupitia CCM, Dkt. John Magufuli kwenye Uwanja wa MajiMaji mjini Songea

 Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu nchini,  Amon Mpanju akiwashutumu viongozi wa upinzani akiwemo mgombea urais kupitia Umoja wa Katiba Wananchi Ukawa, Edward Lowassa kwa kitendo chake cha kuwadhihaki walemavu. Mpanju alikuwa akihutubia  katika mkutano wa kumnadi Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. John Magufuli kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea

Mgombea Urais kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Songea mjini kwenye uwanja wa majimaji ambapo aliwaeleza wananchi hao kuwa Serikali yake itafanyakazi kwa ajili ya maendeleo ya watanzania.
GPL
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top